• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Video ya Li Ziqi yaigwa na blogger wa nchi za nje na kutangazwa kupitia mtandao wa Internet

    (GMT+08:00) 2020-07-27 10:20:05


    Li Ziqi anajulikana sana nchini na nje ya nchi kupitia mtandao wa Internt, kwa kufundisha watu namna ya kupika chakula cha kichina kwa njia ya jadi kupitia mtandao wa kijamii. Alianza kupiga video fupi kuanzia mwaka 2015, na kujulikana nje ya China kuanzia mwaka 2018. Hivi karibuni, watumiaji wa mtandao wa Internet wamegundua kuwa, blogger mmoja wa Vietnam alimwiga Li Ziqi kupanga vipindi vyake vya video kupitia mtandao wa Internet, wakiona kuwa hatua hii imekiuka hakimiliki ya ubunifu, pia wanaona baadhi ya watu wa nchi za nje wanaona kuwa Li Ziqi ni mVietnam, hali ambayo inawakasirisha.

    Lakini wanasheria wamesema, ni jambo lenye utatanishi kwa kuthibitisha kama video hizo zimekiuka hakimiliki ya ubunifu, na kutokana na kuwa kitendo hicho kinatokea nje ya nchi, inapaswa kufuata kanuni za kimataifa za ukiukaji wa hakimiliki na makubaliano yaliyosainiwa kati ya nchi hizo mbili, hali ambayo inaleta utatanishi makubwa.

    Watumiaji wengine wa mtandao wa Internet wanaona hali hii si mbaya, kwani imeonesha kuwa Li Ziqi ambaye anaeneza utamaduni wa China ana ushawishi mkubwa duniani. Video za Li Ziqi zinaonesha wazi utamaduni wa jadi wa kichina, na sura mpya ya maisha ya wakulima nchini China, hali ambayo ni vigumu kwa waigaji wa nchi za ng'ambo kuelewa vizuri na kuonesha undani wa utamaduni huo na maisha ya watu wa China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako