• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mfanyakazi wa usambazaji wa vifurushi awaokoa watu sita kwa kuachangia viungo vya mwili wake baada ya kufariki

    (GMT+08:00) 2020-08-12 15:01:09

    Mwanamume mwenye umri wa miaka 25 aliyekuwa anafanya kazi ya usambazaji wa vifurushi alifariki kutokana na ajali. Wazazi wake waliamua kuchangisha viungo vyake, na kuwaokoa wagonjwa sita. Walisema ingawa mtoto wao amekufa, lakini anaweza kuwaokoa maisha ya watu wengine.

    Mwanamume huyo anayeitwa Chen Jie alitoka wilaya ya Yichen, mkoani Shanxi, aliwahi kufanya kazi ya kusambaza vifurushi katika miji ya Beijing na Suzhou. Alifanya kazi kwa bidii. Mdogo wake alikumbuka kuwa, kwa kawaida Chen Jie alifanya kazi hadi saa saba usiku, wakati wtu wengine wamelala. Wazazi wake pia walisema mtoto wao alijitahidi sana na kutotaka kuwafanya wawe na wasiwasi.

    Tarehe 28 Mwezi Juni Chen Jie alifariki kwa kuzama kwenye maji. Kutokana na Chen Jie kuwa mtu mwenye moyo mwema wa kuwasaidia wengine, na aliwahi kuchangia damu bila malipo mara kwa mara alipofanya kazi za vibarua mjini Beijing, hivyo wazazi wake waliamua kuchangia viungo vyake ili kuwaokoa wengine.

    Chen Jie alichangia moyo, figo, na kuwaokoa watu sita. Baada ya kupata habari hiyo, watu wengi wameguswa na kitendo hicho, wakiona kuwa maisha ya Chen Jie yamedumishwa kwa njia nyingine.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako