• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • APP Ya Kwanza ya Kuripoti Uhalifu Dhidi Ya Vijana

    (GMT+08:00) 2020-09-03 20:59:45


    Hivi karibuni App maalumu ya kwanza ya kuripoti uhalifu dhidi ya vijana imezinduliwa mjini Chongqing. App hiyo iliyobuniwa kwa pamoja na Idara ya kuendesha mashtaka na idara ya polisi ya wilaya ya Jiulongpo mjini Chongqing, hivi sasa inafanyiwa majaribio mtandaoni.

    App hiyo inawawezesha watu kuwasilisha ushahidi wa picha au video kwa polisi unaohusiana na uhalifu dhidi ya vijana, lakini pia inazingatia kulinda faragha ya watu waliotoa ripoti na vijana waliohusika kwenye uhalifu. Hivi sasa wafanyakazi wa idara za serikali, shule, taasisi za mafunzo, taasisi za afya, hoteli na mashirika mengine yanahusiana kwa karibu na vijana katika wilaya ya Jiulongpo wanatakiwa kuweka App hiyo kwenye simu zao za mkononi, ili kutekeleza vizuri wajibu na majukumu yao ya kugundua na kuripoti uhalifu dhidi ya vijana.

    Ripoti yoyote inayowasilishwa kupitia APP hiyo inapokewa na kushughulikiwa na idara ya polisi ya wilaya ya Jiulongpo, na watu waliowasilisha ripoti wanapewa majibu ndani ya siku tatu, na kuarifiwa michakato na matokeo ya kesi ndani ya miezi mitatu, hatua ambazo zote zinasimamiwa kwa karibu na idara ya kuendesha mashtaka.

    Mbali na kuripoti uhalifu, App hiyo pia ina sehemu maalumu ya kutoa mafunzo kwa njia ya video na makala kuhusu namna ya kuwakinga vijana dhidi ya uhalifu, kuchambua sera husika na kesi za mfano zilizoripotiwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako