Xinjiang ina idadi ya wakazakh kiasi cha milioni 1.2, wengi wao wanaishi kwenye jimbo linalojiendesha la kabila la wakazakh, sehemu ya kaskazini ya Xinjiang. Kabila la wakazakh lina lugha na maandishi yake yenyewe.
Wengi wa watu wa kabila hilo ni wafugaji, ambao wanahamahama kwa kufuatana na hali ya malisho katika majira mbalimbali ya mwaka isipokuwa baadhi ya wachache alioshughulikia uzalishaji wa mazao ya kilimo na kukaa katika nyumba za kudumu.
Kwenye sehemu za malisho, wafugaji wanaishi katika nyumba za mviringo zilizotengenezwa kwa nguo ya sufu, ambazo zinaweza kuondolewa na kuhamishwa isipokuwa katika majira ya siku za baridi, ambayo wanaishi ndani ya nyumba zilizojengwa kwa udongo zenye mapaa ya bapa. Watu wa kabila la wakazakh wanapenda kula vyakula viliivyotengenezwa kwa maziwa ya ng'ombe, kondoo na mbuzi na kunywa maziwa pamoja na chai yenye maziwa. Kwenye sehemu za malisho wafugaji wanapenda kula nyama na matumbo ya farasi.
Watu wa kabila la wakazakh wanapenda kuwakaribisha wageni kwa ukarimu mkubwa na kuchinja kondoo.
Wanaume kwa wanawake wa kabila la wakazakh wanajua sana kupanda farasi. Vijana wanapenda kupigana mieleka na mchezo wa kushindania kondoo wakipanda kwenye farasi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |