• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Hafla ya kutoa tuzo kwa washindi wa shughuli ya "Xinjiang Through My Lens" yafanyika huko Urumqi, China

    (GMT+08:00) 2012-07-12 15:31:21

    Hafla ya kutoa tuzo kwa washindi wa shughuli ya "Xinjiang Through My Lens" iliyoandaliwa na Radio China Kimataifa na ofisi ya habari ya serikali ya mkoa unaojiendesha wa Xinjiang Uyghur imefanyika leo tarehe 11 usiku huko Urumqi, China. Miongoni mwa watu walioshiriki hafla hiyo ni Mjumbe wa kudumu wa kamati ya Chama cha Kikomunisti cha China cha mkoa huo ambaye pia ni mkurugenzi wa ofisi ya utangazaji Bw. Hu Wei, naibu mkuu wa Radio China Kimataifa Bw. Xia Jixuan, washindi 11 kutoka China na nchi mbalimbali pamoja na waandishi wa habari.

    Mkurugenzi wa ofisi ya habari ya serikali ya mkoa wa Xinjiang Bibi Hou Hanmin amesema, shughuli ya "Xinjiang Through My Lens" itatoa mchango mkubwa katika kuonesha sura ya Xinjiang kwa pande zote na kuufanya mkoa wa Xinjiang,China ujulikane zaidi duniani.

    Naibu mkuu wa Radio China Kimataifa Bw. Xia Jixuan amesema, kutokana na vyombo vikubwa vya habari duniani kufuatilia shughuli hiyo, sura halisi ya mkoa wa Xinjiang imeonekana, ambayo inawafurahisha na kuwavutia wasikilizaji wa China na wa nchi mbalimbali duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako