Mlima unaowaka wenye urefu wa mita 831.7 uko umbali wa kilomita 10 kaskazini mashariki mwa mji wa Turpan. Mlima huo unaundwa na mawe mekundu, na katika lugha ya Kiuyghur, mlima huo unaitwa mlima mwekundu. kila ifikapo majira ya joto, kutokana na jua kali, hewa joto inakwenda juu, ambapo mlima huo unaonekana kama moto unaowaka. Mlima huu ni sehemu yenye joto kali kabisa nchini China, ambapo halijoto inaweza kufikia zaidi ya nyuzi 45, na ardhi halijoto inaweza kuzidi nyuzi 80.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |