• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wasomaji washindi wa Chemsha bongo kwenye mtandao kuhusu " Xinjiang through my lens" watembelea soko kubwa mkoani Xinjiang

    (GMT+08:00) 2012-07-13 16:19:20

    Wasomaji 11 kutoka nchi mbalimbali pamoja na China ambao wamepata ushindi katika chemsha bongo kwenye mtandao wa internet kuhusu " Xinjiang through my lens" walifika Urumuqi tarehe 10, baadaye walitembelea kwa furaha Bazaar yaani soko kubwa la kimataifa la Xinjiang, ambalo pia ni soko kubwa zaidi dunia.

    Kwenye soko hilo watu wanaweza kujionea utamaduni wa kiislamu, majengo, na biashara ya watu wa makabila mbalimbali, ambapo ni sehemu kubwa ya mkusanyiko na maonesho ya bidhaa za utalii mkoani Xinjiang. Washindi hao kutoka nchi mbalimbali wamevutiwa sana na bidhaa nyingi za aina mbalimbali zenye mitindo pekee ya mkoani Xinjiang.

    Usiku wa siku hiyo, washindi hao pia walikwenda katika Jumba la michezo kutazama maonesho ya michezo ya sanaa, na kufurahia sana maonesho ya wasanii wa kutoka makabila madogomadogo ya China. Katika usiku huohuo pia walikwenda kuonja vyakula vitamu vya huko.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako