• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tarehe 13 Julai 2012

    (GMT+08:00) 2012-07-16 11:19:53

    Tumetembelea ziwa la Paradiso (Tianchi); ziwa hili lipo Milimani jirani na jiji la Urumqi.

    Hapa, joto lilikuwa sentigredi 10 (tofauti na jana huko Turpan, sentigredi zaidi ya 45).

    Kwa namna tulivyojionea, haina tofauti sana na Ngorongoro Crater ya Tanzania. Tofauti kubwa ni utunzaji wa eneo, eneo hili limejengewa barabara nzuri ya lami, maji yanayotiririka yameandaliwa njia nzuri ya kutokea na kurembeshwa, kitu kinachomfanya mtalii kuona thamani ya Ziwa hilo na thamani ya fedha aliyotoa kutembelea eneo husika.

    Tanzania inaweza kufanya vema zaidi, baada ya kuona kinachofanywa na wenzetu katika uhifadhi wa vitegauchumi kama hivi, nimetamani sana nasi tuige mfano huu, hatuna sababu ya kutuzuia kwa kuwa uwezo tunao na sababu tunayo.

    Baada ya kutoka Tianchi, tulielekea uwanja wa ndege na safari kuelekea Kanasi ilianza.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako