• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tarehe 14 Julai

    (GMT+08:00) 2012-07-16 11:20:23

    Tumetembelea vivutio kadhaa mjini Kanasi. Tumetembelea Milima ya Hifadhi ya asili ya Kanasi ambapo nako kuna ziwa kama la Tianchi. Tofauti ya maziwa haya ni kuwa, hili lina maji yanayobadilika rangi.

    Tumetembelea pia maziwa mengine madogomadogo mjini Kanasi. Maziwa haya na mito ni kivutio cha kipekee. Misitu yenye miti na maua ya asili, miti mirefu ya kati ya kijani vinaupamba mji wa Kanasi na kuufanya kuonekana ni Paradiso katika mkoa huu wa Xinjiang.

    Aidha, utamaduni wa wakazi wa Kanasi na Hemu ni kivutio kingine ambacho huwezi kukosa kukiongelea. Ilikuwa ajabu kwangu kusikia kuwa kwa wananchi wa Kanasi (kabila la wa-Kazak) hawaruhusiwi kuoa mtu nje ya kabila lao, na endapo mtu wa nje ya kabila lao akitaka kuoana na mtu wa kabila hili lazima asafishwe tumbo kwa kuwa wanaamini kishakula vitu haramu. Kingine kinachofurahisha ni kuwa, endapo wazazi watakuwa wamebahatika kupata watoto wengi (kama watano hivi) na mtoto wa kwanza akawa ni wa kiume, basi mtoto wao huyu akipata mtoto wake wa kwanza si mali yake bali ni zawadi ya wazazi, yaani; mjukuu atawaita babu na bibi yake 'Baba na Mama' lakini baba yake atamwita 'Kaka'.

    Huko Hemu (mbali kidogo na Kanasi mjini), kuna watu 2,000 hivi ambao wamejitenga na wanaishi maisha yao ya kipekee na bado haijabainika asili ya watu hawa ni wapi. Wametukaribisha vizuri na kwa ukarimu mkubwa, ni kijiji kilichojipanga vema na kinachoonekana kujali sana wageni. Watalii wengi wanaenda kujionea watu hawa walioamua kuishi kwa namna ya kipekee eneo moja.

    Kwa ujumla, nimefurahishwa na mkakati wa serikali kwa wananchi wa vijijini kwani kila nyumba (tena nyingine ni mahema tu) ipo katika mradi wa kuzalisha umeme kwa nguvu za jua (sola). Naamini nasi katika Tanzania tunaweza kuiga mfano huu kwa kutumia mamlaka husika (REA).

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako