• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Utamaduni unaong'ara na maendeleo ya mkoa wa Xinjiang (1)

    (GMT+08:00) 2012-08-07 14:58:58

    Mkoa wa Xinjiang una historia ndefu na utamaduni wa kung'ara wa makabila mbalimbali, na tamaduni za makabila madogomadogo zinahifadhiwa na kuenziwa vizuri, fuatilie kipindi cha utamaduni wetu Ijumaa wiki hii.

    Hivi karibuni washindi 10 wa chemsha bongo katika mashindano yalifanyika kupitia mtandao wa internet kuhusu "Xinjiang machoni mwetu" yaliyoandaliwa na Radio China Kimataifa pamoja na serikali ya mkoa wa Xinjiang walikwenda mkoani Xinjiang kutembelea sehemu za Urumqi, Turpan, Kanas, na Ili, ambapo walivutiwa sana na tamaduni za aina mbalimbali na mandhari nzuri ya mazingira ya asili ya mkoa wa Xinjiang.

    Washindi hao kutoka nchi mbalimbali walisiifu sana serikali ya mkoa huo kwa juhudi zake za kuheshimu na kulinda utamaduni wa makabila mbalimbali na dini za watu, pamoja na hali ya watu wa makabila mbalimbali kupiga hatua kwa pamoja katika kujiendeleza ili kujipatia maendeleo kwa pamoja.

    Washindi hao 10 walitoka Uturuki, Tanzania, Iran, Nigeria, Indonesia, Malaysia, Jordan, Misri, Pakistan na Uingereza. Mbali na mshindi kutoka Uingereza, washindi wengine 9 ni waumini wa dini ya Kiislamu. Ingawa walikuwa wanatumia lugha tofauti na lugha za mkoani Xinjiang, watu wa makabila madogomadogo ni waumini wa dini ya kiislamu, hivyo washindi hao walipotembelea mkoani humo, walikuwa wanajiona kama wako nyumbani. Bw. Hassan Rouhvand kutoka Iran alisema:

    "Naona mkoa wa Xinjiang wa China na nchi yangu Iran zinafanana katika mambo mengi ya utamaduni. Wakazi wengi zaidi mkoani Xinjiang ni waumini wa dini ya kiislamu, na Iran ni nchi ya kiislamu, hivyo hakika mkoa wa Xinjiang na Iran zinafanana katika imani ya kidini; aidha katika safari yangu hii mkoani Xinjiang, nimepata fursa ya kuonja vyakula vingi vitamu vyenye umaalum wa Xinjiang, nilishangaa kuona hata mapishi ya vyakula vitamu vya Xinjiang yanafanana na yale ya Iran, kwa mfano, mishikaki ya nyama ya kondoo iliyo maarufu ya Xinjiang inafanana na ile ya nchini Iran. Pia nimegundua kuwa, kwa desturi za waxinjiang, watu wa ukoo mkubwa wanaishi pamoja, hali hii inafanana sana na ile ya nchini Iran, waxinjiang na wairan wanatilia maanani sana familia, na kutilia maanani kuongeza mawasiliano kati ya jamaa na marafiki."

    Katika mkoa wa Xinjiang, kuna misikiti mingi midogo na mikubwa, misikiti hiyo iliwavutia sana washindi hao kutoka nchi mbalimbali, lakini hii ni picha kubwa ya kwanza waliyopata kuhusu mkoa wa Xinjiang. Washindi hao walipotembelea sehemu mbalimbali mkoani humo, walifurahia sana na uchangamfu na ukarimu wa wakazi wa mkoa huo. Huko Ining, mji mkuu wa tarafa inayojiendesha ya wakhazak ya Ili, kaskazini mwa Xinjiang, washindi hao walitembelea nyumba za wakazi wa kabila la wauyghur, nyumba hizo zilijengwa katika miaka 100 iliyopita, ambapo waligundua kuwa, ndani ya kila nyumba, sebule ya kuwapokea wageni ni kubwa zaidi kuliko vyumba vingine, na sebule hizo zote zimepambwa kwa mazulia murua, na kwenye kuta za nyumba zimetundikwa picha zinazopendeza, na kwenye meza kubwa huwekwa matunda mengi na vitoweo vya aina mbalimbali, ili kuwakaribisha wageni. Mshindi kutoka Uturuki Bibi Eda Ozsoy alisema:

    "Nyumba za wakazi wa Xinjiang pamoja na mapambo na mpangilio wa nyumbani vinafanana sana na vile vya nyumbani Uturuki, kwa mfano sisi waturki pia tunapenda sana kuweka mazulia kwenye sakafu ya nyumba, nyumbani kwetu pia tuna sebule na vyumba vya kupokea wageni. Hivyo naona waturuki na waxinjiang wote ni wachangamfu na wakarimu sana."

    Washindi hao kutoka nchi mbalimbali walitembelea sehemu nyingi za mkoani Xinjiang, kila sehemu waliyofika walikaribishwa na wakazi wa Xinjiang wenye uchangamfu na ukarimu, ambao wanawakirimu wageni hao kutoka mbali kwa mvinyo, nyama za kondoo na matunda matamu. Mshindi kutoka Nigeria Bw. Salisu Dawanau alisema:

    "Waxinjiang wana mila na desturi nzuri sana, wote ni wachangamfu na wakarimu, kama nilivyoona mjini Ining, watu wa kabila la wauyghur waliwakaribisha wageni kwa moyo wa dhati, na kuwakirimu kwa uchangamfu sana, mimi nafurahia sana hali hiyo."

    Wakazi wa Xinjiang huwa wanaonesha uchangamfu wao mkubwa katika maonesho ya michezo ya sanaa. Kila maonesho yanapofika kileleni, waimbaji na wachezaji ngoma wa Xinjiang huwaalika jukwaani wageni kuimba nyimbo na kucheza ngoma pamoja nao. Katika maonesho ya ngoma inayoitwa: " Karamu yenye uhondo mkubwa ya Waturpan", Bw. Raja Mohsin Khaid kutoka Pakistan alialikwa kwenda jukwaani kucheza pamoja na bibi arusi aliyefunikwa kwa shela, baadaye alipofurahia kuondoa shela ya bibi arusi, alishangaa na kuona kuwa kumbe bibi arusi kwenye maonesho hayo siyo msichana, bali ni mwanaume aliyeigiza. Alisema:

    "Nilifurahi sana, waxinjiang hao waliimba nyimbo mbalimbali na kucheza ngoma za aina moja moja, kutokana na maonesho yao, nimefahamishwa mengi kuhusu utamaduni wa waturpan wa mkoa wa Xinjiang. Kwa mfano, wanapocheza ngoma ya kumpokea bibi arusi, njiani kuna watu wengi wanaocheza ngoma wakimzunguka bwana arusi, huku wakimtania sana, bwana arusi akitaka kumchukua bibi arusi wake anapaswa kushinda utani wa watu wengi. Kutokana na maonesho ya ngoma ya wauyghur, tunaweza kuelewa utamaduni wa sehemu walipo, hivyo napenda sana ngoma waliyocheza, na pia nafurahia njia yao ya kufanya maonesho ya kuimba nyimbo na kucheza ngoma zao ili kuwafahamisha wageni utamaduni wa Xinjiang."

    Xinjiang ni sehemu ya mkusanyiko wa ustaarabu wa mashariki na wa magharibi tangu enzi na dahari, katika sehemu hiyo wageni kutoka nchi mbalimbali duniani wanaweza kuona alama za tamaduni tofauti za nchi tofauti. Mbali na dini ya Kiislamu, pia kuna wakazi wa Xinjiang ambao ni waumini wa dini ya Kibudha, dini ya kikristo, dini ya Kidao, na dini ya Kisaman, lakini waumini wa dini tofauti wanaishi pamoja katika hali ya masikilizano bila migogoro. Aidha mkoa wa Xinjiang ni sehemu wanayoishi watu wa makabila 47, ambao wanaishi pamoja katika hali ya masikilizano na wanafundishana, huku kila kabila linadumisha mila na desturi zake zenye umaalum wa kipekee. Bw. Remon Fauzi kutoka Indonesia akisema:

    "Nimepata kumbukumbu nyingi ambazo siwezi kuzisahau katika ziara yangu mkoani Xinjiang, China. Katika mkoa huo, nimejionea aina mbalimbali ya utamaduni, maonesho murua ya ngoma walizocheza wenyeji na mapambo mazuri wanayovaa waxinjiang, naona hii ni sababu moja inayofanya mkoa huo uweweze kuwavutia watalii wengi zaidi."

    Kati ya watu wa makabila 47 wanaoishi mkoani Xinjiang, watu wa makabila 13 yakiwemo makabila ya wauyghur, wahan, wakhazak, wahui, waxibo na warussia wanaishi mkoani humo vizazi hadi vizazi tangu enzi na dahari, watu wa makabila hayo wenye bidii na uhodari wameunda historia na utamaduni wao wenye thamani kubwa. Hivi sasa mabaki mengi ya historia na utamaduni yako kila mahali mkoani Xinjiang, na yamekuwa vivutio vinavyowavutia sana watalii. Bw. Mohamed Said kutoka Misri alisema:

    "Katika sehemu ya Turpan tulitembelea pango lenye vinyago elfu moja vya budha, pamoja na mji mkongwe wa Jiaohe, nimejionea historia na utamaduni wa kung'ara uliovumbuliwa na wakazi wa makabila mbalimbali wa mkoa wa Xinjiang, utamaduni wenye historia ndefu umerithiwa na kuendelea kuenziwa hadi sasa. Nilipojionea majengo makubwa ya utukufu katika mji mkongwe wa Jiaohe, nilijiona kama niko nyumbani nchini Misri nikitembelea mabaki ya kale ya kipindi cha mfalme Pharao wa zamani sana."

    Katika mkoa wa Xinjiang, si kama tu kuna historia ndefu na utamaduni wa kung'ara, bali pia kuna mandhari nzuri sana ya mazingira yake ya asili. Eneo la jangwa lenye rangi ya dhahabu, mbuga yenye majani yanayositawi, au maziwa yake yenye maji safi, yote ni vivutio ambavyo si rahisi kupatikana katika sehemu nyingine duniani. Na hali muhimu ya kuwavutia watu ni kwamba, watu wa makabila mbalimbali mkoani humo wanaishi katika hali ya kupatana na mazingira ya asili, ambapo wanafuga ng'ombe na kondoo, kupanda mazao ya kilimo na kupata mavuno ya kutosheleza mahitaji yao katika maisha.

    Bw. Samsul Said kutoka Malaysia anapenda sana mandhari ya mazingira ya asili ya mkoa wa Xinjiang. Alisema:

    "Nilipotembelea mkoani Xinjiang, nimeona kuwa serikali ya huko inatilia maanani sana uhifadhi wa mazingira, inafanya juhudi kubwa kulinda mazingira yao ya asili ili watu wa vizazi hadi vizazi waweze kuona mandhari nzuri ya mazingira ya mkoa huo. Sehemu mbalimbali za mkoa huo zinapata maendeleo mazuri, wakazi wa sehemu hizo ni wakarimu sana, naona wakazi hao pia wanatengeneza sanaa za mikono ili kuziuza kwa watalii, nashauri watalii wengi zaidi watembelee mkoa huo, kwani mazingira na vitu vingi vya mkoani humo ni vya asili, serikali na wakazi wa huko wanajitahidi kuhifadhi mazingira yao."

    Baada ya kutembelea vyombo vya habari na Jumba la makumbusho mkoani Xinjiang, Bw. Said Ihmaidi kutoka nchi ya Jordan alisema:

    "Nimepata picha nyingi kuhusu mkoa wa Xinjiang kufanya juhudi za kuhifadhi lugha na utamaduni wa makabila mbalimbali, nimeona katika vituo vya radio, televisheni na tovuti kwenye mtandao wa internet mkoani Xinjiang kuna matangazo ya vipindi ya lugha za Kiuyghur na Kikhazak za makabila madogomadogo, ili kuwahudumia wakazi wa huko. Katika Jumba la makumbusho ya Xinjiang, kuna sehemu tofauti za maonesho ya kila kabila dogo, ili kuonesha utamaduni, mila na desturi za kila kabila dogo. Juhudi za China katika kuhimiza mshikamano wa kikabila zinastahili kusifiwa na watu."

    Bw. Maxence Melo Mubyazi kutoka Tanzania ni mhandisi wa software, yeye alitembelea Kampuni ya sayansi na teknolojia ya Karlo mjini Urumqi mkoani Xinjiang, alisifu sana juhudi za kampuni hiyo katika kuwaandaa watu wenye ujuzi akisema:

    "Kampuni hiyo imenipa kumbukumbu nyingi, ni kampuni pekee binafusi inayofanya ushirikiano na Kampuni ya Apple. Wafanyakazi wake karibu wote ni vijana kutoka kabila dogo la wauyghur, napongeza sana kazi ya shule ya kampuni hiyo ya kuwaandaa vijana wengi wenye ujuzi wa kompyuta kutoka kabila dogo la wauyghur, baada ya kuhitimu, baadhi ya wanafunzi wanafanya kazi katika kampuni hiyo, wengine wanapata nafasi za ajira katika kampuni nyingine, shule hiyo inawasaidia vijana wa kabila la wauyghur kupata ujuzi wa kazi ili baadaye wapate ajira."

    Katika safari ya siku nane mkoani Xinjiang kwa washindi hao wa mashindano ya "Xinjiang machoni mwetu" yaliyofanyika kupitia mtandao wa internet, washindi hao kutoka nchi mbalimbali wamejionea hali halisi ya mkoa wa Xinjiang, ambayo ni tofauti sana na ile iliyotangazwa na vyombo vya habari vya nchi za magharibi. Katika mkoa huo watu wa makabila mbalimbali wanaishi katika hali ya masikilizano, ambapo utamaduni na imani za dini za makabila mbalimbali unaheshimiwa, mkoa wa Xinjiang wenye historia ndefu na utamaduni unaong'ara unaonekana kuwa na nguvu ya uhai katika kujiendeleza.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako