• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • shairi la Manasi

    (GMT+08:00) 2012-08-13 10:16:18
    Leo tunaendelea na safari yetu mkoani Xinjiang, kaskazini magharibi mwa China, ambapo wanaishi watu wa makabila mengi madogo madogo, kama waUygur, waKirgiz na waMongolia. Kila kabila lina utamaduni wake wenye umaalum wa kipekee, na mashairi ni sehemu muhimu ya utamaduni wa makabila hayo, sababu mashairi yao yanabeba historia, usanii hata lugha ya kabila. Leo katika kipindi hiki tunawafahamisha mashairi ya makabila mawili ya waKirgiz na waMongolia mkoani Xinjiang.

    Unalosikia ni shairi la kabla la waKirgiz liitwalo MANAS, shairi hilo linajulikana kama Encyclopedia ya kabila la Wakirgiz, sababu linaelezea historia, utamaduni na maisha ya kabila hilo. Chimbuko la Shairi la MANAS ni tarafa ya Akqi, wilaya ya Kirgiz, mkoa wa Xinjiang. Katika tarafa hiyo, karibu kila familia ina kitabu cha shairi la MANAS. Watoto wanasikiliza baba na babu wakiimba shairi hilo tangu wanapokuwa na umri mdogo.

    Anayeimba shairi hilo ni mzee Jusufu Mamayi, ambaye anafahamika sana miongoni mwa watu wa kabila la Wakirgiz. Mzee huyo anajua kuimba shairi zima la MANAS, lenye juzuu 8 ambalo lina jumla ya mistari laki 2.3. Hakuna mwingine anayejua zaidi kuimba shairi hilo kuliko yeye.

    Tukimtazama mzee Mamayi, anaonekana kama ni mzee anayesimuliwa kwenye hadithi za watoto, mwenye ndevu, mpole, na macho yake yanaonesha busara aliyonayo. Mzee huyo alianza kujifunza kuimba MANAS tangu alipokuwa mtoto wa miaka 8. Baada ya kufanya mazoezi mengi, alipofikisha umri wa miaka 30, alikuwa ameshakumbuka shairi hilo zima na kuweza kuimba bila kuangalia kitabu.

    Anapoimba MANAS, huimba kwa sauti kubwa bila kufuatwa na upigaji wa muziki kwa vifaa, lakini uimbaji wake wa shairi unagusa sana miyo ya watu.. Waimbaji wengi wa MANAS wanaweza kuimba mchana kutwa, usiku kucha. Mzee Kurmanali mwenye umri wa miaka 69 ni mmoja kati ya waimbaji hao.

    "Nilipokuwa kijana, niliwahi kuimba kwa siku nzima saa 24, lakini sasa nimezeeka, naweza kuimba kwa saa moja tu kila mara."

    Sio tu wanaume, wanawake pia wamejiunga kwenye uimbaji wa shairi hilo. Kuna wanawake wengi walio waimbaji hodari wa MANAS, akiwemo Bibi Goncagul.

    Anapozungumzia jinsi alivyofundishwa uimbaji wa MANAS Goncagul anasema:

    "Nilianza kujifunza uimbaji wa MANAS tangu nilipokuwa na umri wa miaka 13, baba ndiye aliyenifundisha, anapenda niwe mwimbaji wa MANAS na ananisaidia sana. Sioni shida yoyote katika uimbaji wa MANAS."

    MANAS ni shairi ambalo halina maandishi, watu wanapokezana kwa midomo. Ili kurithisha shairi hilo, serikali inaandaa shughuli za uimbaji wa MANAS kila mwaka na kuwahamasisha watu washirikiane, na pia imeongeza somo la uimbaji wa MANAS kwenye mitaala ya masomo ya shule za msingi. Bostan, ambaye mtoto wake mwenye umri wa miaka 12 anasoma katika shule ya msingi katika tarafa ya Akqi, anafurahia mtoto wake kufundishwa uimbaji wa MANAS.

    "MANAS ni Encyclopedia ya WaKirgiz, watoto waweza kujifunza lugha ya kabila lao kupitia somo la uimbaji shairi hili, pia wanaweza kufahamu mila na desturi, historia na utamaduni wa kabila letu. "

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako