• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • shairi la Janggar

    (GMT+08:00) 2012-08-13 10:20:29
    MANAS ni shairi la kabila la waKirgiz. Hebu sasa tugeukie kabila lingine la waMongolia, wamongolia pia wana shairi lao liitwalo JANGGAR. Shairi hilo linaelezea hadithi za kiongozi wa zamani wa kabila hilo Janggar. Kiongozi huyo aliwaongoza watu wa kabila lake kupambana na wavamizi, kulinda malisho yao na kuwaletea watu wake maisha mazuri.

    Kama ilivyoelezwa kwenye shairi hilo, Janggar ni shujaa kijana mwenye nguvu na busara, alionekana kuwa ni mtanashati mwenye umri wa miaka 25 hivi, na hazeeki kabisa.

    Je, kiongozi huyo ni mtu halisi katika historia? Profesa Jamcha kutoka Chuo Kikuu cha Xinjiang, ambaye ni mtafiti wa shairi la JANGGAR anaona kuwa, Janggar si jina la mtu fulani, bali ni kwamba mashujaa wote wa kabila la waMongolia wanaweza kuitwa kuwa Janggar.

    "Neno hili Janggar haliko katika msamiati wa lugha ya kabila la waMongolia, bali ni neno la lugha ya kiajemi, maana yake ni 'Aliyeiteka dunia'. Wataalamu wengi wanaona Janggar ni mashujaa walioibuka kati ya karne ya 12 na 14. Msomi kutoka Russia amesema, shairi la JANGGAR ni historia iliyopambwa kwa usanii na hadithi zilizobuniwa, ili kuwasifu mashujaa wa kabila la Wamongolia."

    Kama lilivyo shairi la MANAS, shairi la JANGGAR linachukuliwa pia kama encyclopedia ya kabila la Wamongolia. Shairi hilo linaelezea historia ya kabila hilo, utamaduni wao na jinsi wanavyoishi kizazi baada ya kizazi. Sauti-9

    Mzee Sharniman wa tarafa ya Hejing, ni mrithi wa shairi hilo. Mzee huyo anajua kuimba sura zote 26 za shairi hilo. Na mchango wake kwa shairi hilo sio tu kujua namna ya kuimba, bali pia kuwafundisha wengine kuimba. Ana wanafunzi 53 nyumbani, kati yao wanane wamejua vizuri kuimba. Mbali na kufundisha nyumbani, kila wiki mzee Sharniman anakwenda katika shule ya nne ya sekondari ya tarafa ya Hejing kufundisha darasani.

    "Watoto hao wanapenda kujifunza uimbaji wa JANGGAR, wengi wao wameniambia wanataka kuwa waimbaji wa JANGGAR. Kwa hiyo nina matumaini kuhusu mustakbali wa kurithishwa na kuenziwa kwa usanii huu."

    Hata hivyo, kama ulivyo usanii wa aina nyingine ambao unaanza kutoweka siku hizi, kurithishwa na kuenziwa kwa shairi hilo kunakabiliwa na changamoto nyingi. Mzee Sharniman anasema, hili ni jambo ambalo linahitaji nia thabiti, na nia thabiti ndiyo mafunzo tuliyopata kutoka kwa shairi lenyewe.

    "Jangger ana moyo wa kutokubali kushindwa, anapenda kukabiliana na changamoto. Tusipokuwa na moyo huu, hatuwezi kufaulu kwenye jambo lolote katika maisha yetu."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako