7: Majengo

Maelezo kwa Ufupi

Majengo ya Jadi ya Kichina

Majengo ya jadi ya Kichina ni sehemu muhimu ya utamaduni mkubwa unaong'ara wa China, aina za majengo hayo pamoja na ya Kimagharibi na ya Kiarabu ni aina tatu muhimu za majengo duniani.

Majengo ya jadi ya Kichina ni majengo pekee yanayojengwa kwa mbao, na yanaonesha fikra za watu wa China kuhusu maadili ya jamii na mtazamo wa uzuri. Kutokana na utamaduni wa jadi, aina za majengo ya Kichina zimegawanyika kama ifuatayo: majengo yanayotukuza mamlaka ya kifalme, majengo hayo yanaonekana zaidi katika ujenzi wa makasri na mpango wa ujenzi wa mji mkuu; mkazo unatiliwa zaidi kwenye uzuri wa jumla wa seti ya majengo, na kuyafanya majengo kwenye pande mbili za mstari wa katikati yalingane, na kulingana na mazingira ya kimaumbile.

Mbali na majengo ya kabila la Wahan, kuna aina nyingi za majengo ya makabila madogo madogo ambayo zinachangia uzuri wa mfumo wa ujenzi wa Kichina.

Majengo hayo yamegawanyika katika aina tano, nazo ni majengo ya kasri, majengo ya mahekalu, majengo ya bustani na majengo ya makaburi.

Katika historia ya China, sanaa na ufundi wa majengo ya Kichina iliwahi kuathiri ujenzi wa majengo ya Kijapan, Kikorea, Kiviet Nam na Kimongolia. Leo majengo ya Kichina licha ya kuendelea na mtindo wake wa jadi pia yameingiza sanaa za majengo ya Kimagharibi na kuziendeleza.


1 2 3 4 5 6