7: Majengo

Majengo ya Siku Hizi

Muhtasari wa Majengo ya Kisasa

Majengo ya kisasa yanamaanisha majengo yaliyojengwa kuanzia katikati ya karne ya 19 hadi sasa.

Tokea vita vya kasumba vya mwaka 1840 hadi Jamhuri ya Watu wa China kuasisiwa mwaka 1949, majengo yenye mtindo wa Kichina na wa Kimagharibi yalitokea nchini China. Katika kipindi hiki majengo ya mtindo wa Kichina yanaendelea kuwa mengi, lakini nyumba za michezo, mahoteli, maduka, na maduka makubwa yalikuwa hujengwa kwa mchanganyiko wa mitindo ya Kichina na ya Kimagharibi na majengo ya aina ya Kimagharibi yalitokea katika miji ya Shanghai, Tianjin, Qingdao na Harbin kwenye sehemu zilizokodiwa na nchi za nje, na pia majengo ya ubalozi, benki za nchi za nje na mahoteli na klabu za nchi za nje zilitokea katika miji hiyo.

Baada ya Jamhuri ya Watu wa China kuasisiwa mwaka 1949, ujenzi umeingia katika kipindi kipya cha kihistoria, kutokana na jinsi uchumi ulivyoendelea kwa haraka ujenzi wa majengo uliongezeka. Katika kipindi hiki majengo makubwa 10 yenye mapaa ya aina ya kasri la kifalme yalijengwa katika mwaka wa maadhimisho ya miaka kumi tokea Jamhuri ya Watu wa China iasisiwe. Tokea miaka ya 80 ya karne iliyopita, majengo yameanza kuwa na aina kwa aina.

Mifano ya Majengo ya Kisasa nchini China

Hoteli ya Heping mjini Shanghai

Hoteli ya Heping mjini Shanghai ilijengwa mwaka 1929, ni jengo la aina ya Gothic ya Italia. Urefu wake ni mita 77 na ghorofa 12. Ukuta kwa nje ulijengwa kwa mawe ya itale na kwa ndani nguzo na sakafu ilijengwa kwa marumaru. Hilo ni jengo la fahari katika Mashariki ya Mbali.

Kaburi la Dkt. Sun Yat-sen

Dkt. Sun Yat-sen ni mtangulizi mkubwa wa mapinduzi ya kidemokrasia nchini China, kaburi lake lilijengwa mlimani nje kidogo ya mji wa Nanjing. Majengo kutoka chini ya mlima mpaka juu ni uwanja, milango ya mawe, ngazi, lango la kaburi, vibanda vya mawe yenye maandishi, ukumbi wa kutoa heshima na ukumbi wa jeneza. Mtindo wa majengo ya kaburi la Dkt. Sun Yat-sen ni muunganisho wa mtindo wa jadi wa Kichina na wa Kimagharibi. Kaburi hilo linasifiwa kuwa ni "kaburi la fahari katika historia ya siku hizi nchini China".

Kaburi la Dkt. Sun Yat-sen

Ukumbi Mkuu wa Umma

Ukumbi Mkuu wa Umma uko katika upande wa magharibi wa uwanja wa Tian An Men, ni mahali viongozi wa taifa na umma wanaposhughulika na mambo ya siasa, na pia ni moja kati ya majengo makubwa nchini China. Ukumbi huo ulijengwa mwaka 1959, eneo lake ni mita za mraba laki 1.7. Ukumbi Mkuu wa Umma waonekana kwa ufahari, na unalingana na mazingira ya uwanja wa Tian An Men. Mlango wa mbele unatazama uwanja wa Tian An Men, na juu ya mlango huo inabandikwa nembo ya taifa, na pande mbili za mlango huo ni nguzo 12 ya marumaru yenye urefu wa mita 25. Baada ya kuingia kwenye mlango huo kuna ukumbi mkubwa, nyuma ya ukumbi huo ni ukumbi wa kufanyia mkutano wenye eneo la mita 76 kwa upana na mita 60 kwa urefu, kwenye upande wa kulia wa ukumbi huo wa mkutano ni ukumbi wa karamu wenye nafasi 5,000. Ndani ya Ukumbi Mkuu wa Umma kuna kumbi zaidi ya mia moja, na kila ukumbi una uzuri wake wa kipekee.

Hoteli ya Xiangshan

Hoteli hiyo ilijengwa mwaka 1982, ilisanifiwa na Bei Yuming, msanifu mkubwa wa Marekani mwenye asili ya China. Hoteli hiyo imejengwa mlimani kwa mtindo wa kale wa Kichina. Mwaka 1984 hoteli hiyo ilipata tuzo ya sifa ya Shirikisho la Ujenzi la Marekani.


1 2 3 4 5 6