8: Elimu, Sayansi na Teknolojia

Vyuo Vikuu Maarufu vya China

Hali ya Vyuo Vikuu Nchini China kwa Muhtasari

Katika miaka ya hivi karibuni, vyuo vikuu vya kitaifa vya China vimeongeza wanafunzi kwa kiasi kikubwa. Hivi sasa idadi ya wanafunzi wanaosoma katika vyuo vikuu imeongezeka kwa mara kadhaa kuliko ile ya mwaka 1998, hadi kufikia milioni 20, ambao wanachukua asilimia 17 ya vijana wa rika moja.

Hivi sasa China ina vyuo vikuu zaidi ya 3000, kati ya hivyo, zaidi ya 1300 ni vyuo vikuu vya kawaida, zaidi ya 1200 vinaendeshwa na watu binafsi, vingine ni vya watu wazima. Elimu ya juu nchini China ina madaraja ya vyuo vya shahada, vyuo vikuu, mafunzo ya shahada ya pili na ya udaktari.

Kwa kawaida, wanafunzi wa vyuo vya shahada wanatakiwa kusoma kwa miaka mitatu, na wanafunzi wa vyuo vikuu watasoma kwa miaka minne, na wanafunzi wa shahada ya pili na ya udaktari wanatakiwa kujisoma kwa miaka miwili au mitatu.

Vyuo vikuu vya kitaifa vinatoa mchango mkubwa katika elimu ya juu nchini China, vyuo vikuu vyote vya elimu za mseto na utafiti vinaendeshwa na taifa. Katika miaka ya hivi karibuni, vyuo vikuu vinavyoendeshwa na watu binafsi vinaongezeka kwa haraka, baadhi ya vyuo hivyo pia vina kiwango kikubwa, lakini bado vina tofauti na vile vya taifa katika sifa na taaluma.

Chuo Kikuu cha Beijing

Chuo Kikuu cha Beijing ni chuo kikuu cha elimu za mseto cha kitaifa ambacho kinajulikana nchini kutokana na kiwango kikubwa cha utoaji elimu na utafiti. Chuo hicho ilianzishwa mwaka 1898, ni kimoja cha vyuo vikuu vyenye historia ndefu nchini China.

Baada ya maendeleo ya miaka mia moja, hivi sasa Chuo Kikuu cha Beijing kina sehemu tano za utamaduni, sayansi ya jamii, sayansi, upashanaji habari na uhandisi na utibabu. Kina tovuti 42, vituo 216 vya utafiti, na hospitali 18 za kufundishia zilizo chini yake. Kozi za chuo kikuu hicho za Kichina, lugha za kigeni, historia, fizikia na viumbe zinajulikana zaidi nchini China.

Chuo Kikuu cha Beijing sasa kina wanafunzi zaidi ya elfu 15 wa shahada ya kwanza, na wanafunzi elfu 12 wa shahada ya pili na ya udaktari, pia kimewavutia wanafunzi wengi wa nchi za nje. Maktaba ya Chuo Kikuu cha Beijing ni maktaba kubwa kabisa cha chuo kikuu katika bara la Asia, ina vitabu milioni 6.29. Kama ukitaka kufahamu habari nyingi zaidi kuhusu Chuo Kikuu cha Beijing, soma tovuti ya chuo hicho : http://www.pku.edu.cn/

Chuo Kikuu cha Tsinghua

Chuo Kikuu cha Tsinghua mjini Beijing ni chuo kikuu cha kitaifa maarufu kabisa cha utafii na elimu za mseto kinachojulikana kwa kozi za sayansi na uhandisi, kina historia ya miaka mia moja hivi, ni moja ya vituo muhimu vinavyowaandaa wasomi wenye kiwango cha juu nchini China.

Hivi sasa, Chuo Kikuu cha Tsinghua kina vitivo 44 katika taasisi 11 za sayansi, ujenzi, uhandisi wa hifadhi maji, uhandisi wa mitambo, sayansi na teknolojia ya upashanaji habari, utamaduni na sayansi ya jamii, usimamizi wa uchumi, sheria, uchoraji picha, usimamizi wa mambo ya umma na kadhalika. Kozi zake za ujenzi, kompyuta, magari, fizikia na nyinginezo zinajulikana sana nchini China. Katika miaka 20 iliyopita, Chuo Kikuu cha Tsinghua kinajiendeleza kuwa chuo kikuu cha mseto wa elimu, kimeongeza kozi za usimamizi, Kichina na uandishi wa habari, na kiko mbioni kuanzisha chuo cha utibabu.

Hivi sasa Chuo Kikuu cha Tsinghua kina wahadhiri na maprofesa 7100, wanafunzi zaidi ya elfu 20, ambapo wanafunzi elfu kumi kati yao wa shahada ya pili na ya utakdari. Wanafunzi wengi wa wanafunzi wa ng'ambo wanapenda kusoma katika chuo kiuu hicho.

Chuo Kikuu cha Tsinghua kinajulikana nchini na duniani kutokana na kiwango cha juu cha utaalamu na ubora wa elimu. Kama ukitaka kufahamu habari nyingi zaidi kuhusu Chuo Kikuu cha Tsinghua, soma tovuti: http://www.tsinghua.edu.cn

Chuo Kikuu cha Fudan

Chuo Kikuu cha Fudan kiko mjini Shanghai, mji mkubwa kabisa wa viwanda na biashara nchini China, ni moja ya vyuo vikuu maarufu vya mseto wa elimu nchini China, pia ni moja ya vyuo vikuu vyenye historia ndefu nchini China.

Hivi sasa chuo kikuu hicho kina kozi nyingi ambazo ni pamoja na utamaduni, sayansi za jamii na maumbile, teknolojia, usimamizi na utibabu. Kina vitivo 72 katika taasisi 15 ambavyo ni pamoja na chuo cha uandishi wa habari, chuo cha sayansi ya maisha, chuo cha utibabu cha Shanghai na chuo cha software. Pia kina taasisi 65 za utafiti, na vituo 91 vya utafiti unaoshughulikia zaidi ya kozi moja. Hivi sasa Chuo Kikuu cha Fudan kimekuwa moja ya vituo vyenye sifa nzuri ya kitaaluma duniani, kimeanzisha ushirikiano na maingiliano na vyuo vikuu na taasisi za utafiti zaidi ya 200 kutoka nchi na sehemu 30 hivi.

Chuo Kikuu cha Fudan sasa kina wanafunzi elfu 25, na wanafunzi 1650 wa nchi za nje. Kama ukitaka kufahamu habari nyingi zaidi kuhusu chuo kikuu hicho, soma tovuti yake:http://www.fudan.edu.cn/

Chuo Kikuu cha Ualimu cha Beijing

Chuo Kikuu cha Ualimu cha Beijing kilianzishwa mwaka 1902, ni chuo kikuu cha kwanza cha ualimu katika historia ya China, na pia ni chuo kikuu maarufu kati ya vyuo vya ualimu nchini China.

Katika chuo kikuu hicho kuna chuo cha elimu, chuo cha kuwaandaa walimu, chuo cha lugha ya Kichina na vyuo vingine vipatavyo 15 kwa jumla vyenye masomo 48. kati ya masomo hayo somo la elimu, saikolojia, elimu kabla shule ya msingi zinajulikana zaidi.

Katika chuo kikuu hicho kuna wafanyakazi na walimu karibu 2500, wanafunzi zadi ya elfu 20, na wanafunzi kutoka nchi za nje 1000.

Katika miaka ya karibuni licha ya kuendeleza masomo ya ualimu, chuo kikuu hicho kimestawisha zaidi masomo mengine yasiyo ya ualimu, pia kimeanzisha mafunzo ya kuwapatia walimu wa kazini ujuzi zaidi.

http://www.bnu.edu.cn/

Chuo Kikuu cha Nanjing

Chuo Kikuu cha Nanjing kiko katika mji wa Nanjing, mji mkuu wa mkoa wa Jiangsu, kinajulikana zaidi kwa kozi za sayansi na uhandisi, na ni moja ya vyuo vikuu maarufu nchini China.

Hivi sasa Chuo Kikuu cha Nanjing kina vitivo 43 katika taasisi 16 ambavyo ni pamoja na chuo cha fasihi, chuo cha sayansi, chuo cha jiografia na chuo cha utibabu, kina walimu 2000 na wanafunzi elfu 31, miongoni mwa wanafunzi hao, wanafunzi zaidi ya 8500 wanasomea shahada ya pili na ya udaktari.

Chuo Kikuu cha Nanjing ni moja ya vyuo vikuu vinavyofanya shughuli nyingi za maingiliano ya taaluma ya kimataifa. Maprofesa wengi waliopata tuzo ya Nobel wakiwemo Li Zhengdao, Ting Zhaozhong, Yang Zhenning, Glashow, Robert A. Mundell wamekuwa maprofesa wa heshima wa Chuo Kikuu cha Nanjing. Kama ukitaka kufahamu habari nyingi zaidi kuhusu Chuo Kikuu cha Nanjing, soma tovuti:http://www.nju.edu.cn/

Chuo Kikuu cha Zhongshan

Chuo Kikuu cha Zhongshan kiko katika mji wa Guangzhou, mji mkuu wa mkoa wa Guangdong, kusini mwa China, ni chuo kikuu mchanganyiko wa elimu. Chuo kikuu hicho kilianzishwa mwaka 1924 na Bwana Sun Yat-sen , kiongozi maarufu wa mapinduzi ya demokrasia ya China.

Chuo Kikuu cha Zhongshan kina kozi 79 katika taasisi 19 ambazo ni pamoja na taasisi ya utamaduni, taasisi ya Lingnan, taasisi ya hisabati na sayansi ya kompyuta na taasisi ya utibabu. Chuo kikuu hicho kina maabara na kituo cha utafiti chenye zana za kisasa. Chuo kikuu hicho kina wanafunzi elfu 41 wa elimu aina mbalimbali, kati ya hao kuna wanafunzi elfu 17 wa shahada ya kwanza, wanafunzi 5440 wa shahada ya pili, wanafunzi 1970 wa shahada ya udaktari, na wengine 450 kutoka nchi za nje. Sehemu mpya ya Chuo cha Lingnan cha Chuo Kikuu cha Zhongshan ina mandhari nzuri na zana za kisasa, inasifiwa kuwa ni moja ya sehemu zinazopendeza zaidi katika vyuo vikuu nchini China. Maktaba ya Chuo Kikuu cha Zhongshan ni moja ya maktaba zenye vitabu vingi katika sehemu ya kusini mashariki China. Ukitaka kufahamu habari nyingi zaidi kuhusu Chuo Kikuu cha Zhongshan, soma tovuti yake:http://www.zsu.edu.cn/

Chuo Kikuu cha Wuhan

Chuo Kikuu cha Wuhan kiko mjini Wuhan, mji mkuu wa mkoa wa Hubei katikati ya China. Hiki ni moja ya vyuo vikuu vya mseto wa elimu na utafiti chenye kozi nyingi. Chuo Kikuu cha Wuhan kina kozi 105 katika vitivo 11 vya falsafa, uchumi, sheria, elimu, fasihi, historia, sayansi, uhandisi, kilimo, utibabu na usimamizi. Chuo kikuu hicho kina walimu zaidi ya 5000 na waanfunzi zaidi ya elfu 45, miongoni mwao kuna wanafunzi elfu 12 wa shahada ya pili na ya udaktari. Katika miaka ya hivi karibuni, Chuo Kikuu cha Wuhan kimewaalika wasomi na wanasiasa maarufu 300 wa nchini na ng'ambo kuwa maprofesa wake wa heshima, na kuanzisha ushirikiano na maingiliano na vyuo vikuu na taasisi zaidi ya 200 za utafiti wa kisayansi za nchi na sehemu zaidi ya 60.

Chuo Kikuu cha Wuhan iko kwenye mteremko wa mlima wa Luojia, inasifiwa kuwa ni moja ya chuo kikuu cha kupendekeza zaidi nchini China. Ukitaka kufahamu habari nyingi zaidi kuhusu Chuo Kikuu cha Wuhan, soma tovuti ya mtandao: http://www.whu.edu.cn/

Chuo Kikuu cha Zhejiang

Chuo Kikuu cha Zhejiang kiko mjini Hanzhou, mji mkuu wa mkoa wa Zhejiang, kusini mashariki mwa China. Hiki ni moja ya vyuo vikuu vya utafiti vyenye kiwango kikubwa na kozi nyingi zaidi nchini China, na kinajulikana duniani.

Kozi za Chuo Kikuu cha Zhejiang ni pamoja na falsafa, uchumi, sheria, elimu, fasihi, historia, sayansi na uhandisi, kilimo, matibabu na usimamizi. Kuna kozi 108 za shahada ya kwanza. Hivi sasa Chuo Kikuu cha Zhejiang kina walimu zaidi ya 8700 na wanafunzi zaidi ya elfu 40, kati ya wanafunzi hao, wanafunzi 9700 wanasomea shahada ya pili, wanafunzi 4200 wanasomea shahada ya udaktari na wanafunzi zaidi ya 1000 kati ya hao wanatoka nchi za nje.

Chuo Kikuu cha Zhejiang kimepata mafanikio makubwa ya taaluma katika kozi za uchumi, sheria na sayansi. Eneo la jumla la maktaba yake linafikia mita za mraba elfu 59, ina vitabu milioni 5.91, ni moja ya maktaba kubwa ya vyuo vikuu vyenye mchanganyiko wa elimu nchini China. Ukitaka kufahamu habari nyingi zaidi kuhusu Chuo Kikuu cha Zhejiang, soma tovuti yake:http://www.zju.edu.cn/

Chuo Kikuu cha Sichuan

Chuo Kikuu cha Sichuan kiko mjini Chengdu, mji mkuu wa mkoa wa Sichuan, kusini magharibi mwa China, hiki ni chuo kikuu chenye kozi nyingi na kiwango kikubwa katika sehemu ya kusini magharibi ya China. Hivi sasa, kinatoa mafunzo yanayohusiana na sekta 9 za utamaduni, sayansi ya jamii na maumbile, uhandisi na utibabu.

Hivi sasa Chuo Kikuu cha Sichuan kina vitivo 30 vyenye kozi 118, kina walimu na wafanyakazi 11,357 na wanafunzi elfu 43.9, kati yao wanafunzi 10,000 wanasomea shahada ya pili na 2,740 wanasomea shahada ya udaktari, na wanafunzi 653 wanatoka nchi za nje na sehemu ya Macao na Hongkong. Ukitaka kufahamu habari nyingi zaidi kuhusu chuo kikuu hicho, soma tovuti yake: http://www.scu.edu.cn/

Chuo Kikuu cha Mawasiliano cha Shanghai

Chuo Kikuu cha Mawasiliano cha Shanghai ni moja ya vyuo vikuu muhimu nchini China, kilianzishwa mwaka 1896. Hivi sasa chuo kikuu hicho kina vitivo 21 vya uhandisi wa meli na upashanaji bahari, uhandisi wa mashine na nishati na kadhalika, vina kozi 55 kama vile sayansi, uhandisi, utamaduni, usimamizi, kilimo, uchumi, sheria na elimu. Kinakaribia kiwango cha kwanza duniani katika elimu kadhaa kama vile mawasiliano ya simu na upashanaji habari, uhandisi wa meli na bahari, udhibiti unaojiendesha, nyenzo zinazochanganywa na kadhalika.

Hivi sasa, chuo kikuu hicho kina wanafunzi elfu 14 wa shahada ya kwanza, wanafunzi zaidi ya 7000 wa shahada ya pili na ya udaktari na wanafunzi zaidi ya 1600 kutoka nchi za nje. Katika miaka mingi iliyopita, Chuo Kikuu cha Mawasiliano cha Shanghai kimewaandaa wasomi zaidi ya laki moja ambao ni pamoja na wanasiasa, wanaharakati wa mambo ya kijamii, wanaviwanda, wanasayansi, maprofesa na wataalamu. Ukitaka kufahamu habari nyingi zaidi kuhusu Chuo Kikuu Cha Mawasiliano Cha Shanghai, soma tovuti ifuatayo:http://www.sjtu.edu.cn/


1 2 3 4 5 6 7