14: Historia

Vitabu Maarufu vya Historia ya China

Mbinu za Kijeshi za Sunzi

Mbinu za kijeshi za Sunzi ni maandiko makubwa mashuhuri ya kele ya China kuhusu nadharia ya kijeshi, na ni moja ya maandishi yenye athari kubwa zaidi na kuenezwa kwenye maeneo makubwa zaidi duniani. Mawazo ya mbinu na falsafa iliyoko kwenye maandiko hayo yanatumika sana katika maeneo mbalimbali yakiwemo ya kijeshi, kisiasa na kiuchumi. Kitabu cha "Mbinu za Kijeshi za Sunzi" kiliandikwa miaka 2,500 iliyopita na ni maandiko ya nadharia ya kijeshi cha mapema zaidi duniani, ambayo ni mapema kwa miaka 2,300 kuliko kitabu cha "On War" kilichoandikwa na Clausewitz wa Ulaya.

Mwandishi wa kitabu cha "Mbinu za Kijeshi za Sunzi" ni Su Wu ambaye alikuwa bingwa wa kijeshi katika kipindi cha Chunqiu na kuheshimiwa kuwa "mwanaelimu mkuu wa kijeshi" katika kipindi cha Chunqiu. Wakati ule Sun Wu ili kukwepa vita alikimbilia nchi ya Wu na kuteuliwa kuwa jemadari wa mfalme wa Wu, alishinda jeshi lenye askari laki 2 la nchi ya Chu kwa kutumia jeshi lake lenye askari elfu 30. Sun Wu alijumlisha uzoefu wa kivita hadi miaka ya mwisho ya kipindi cha Chunqiu na kutoa mfumo kamili wa nadharia ya mambo ya kijeshi. Kitabu cha "Mbinu za Kijeshi za Sunzi" kina maneno zaidi ya 6,000 na chenye makala 13, ambazo kila makala inaeleza mada moja. Wazo la kitabu hicho ni njia bora zaidi katika mambo ya kijeshi ni kupata ushindi kwa kutumia mbinu za kisiasa, halafu ni mbinu za kidiplomasia, za kutumia nguvu za kijeshi na mwisho ni kuteka mji wenye ngome. Hivyo bingwa wa kivita anapaswa kujua yali halisi za adui na kupata habari kwa kutumia majasusi. Kitabu cha "Mbinu za Kijeshi za Sunzi" ni chenye mawazo ya kifalsafa. Kwa mfano maneno ya "Ukijua hali halisi zako na za adui, utashinda daima" sasa yanatumiwa hata na watu wa kawaida. Kitabu hicho cha "Mbinu za Kijeshi za Sunzi" kimechapishwa kwa lugha za aina 29 zikiwemo za Kingereza, Kirusi, Kijerumani na Kijapan. Vyuo vya nchi nyingi duniani vinatumia kitabu cha "Mbinu za Kijeshi za Sunzi" kama kitabu chao cha kiada. Habari zinasema kuwa katika vita vya ghuba mwaka 1991, pande mbili zilizopigana zote zilifanya uchunguzi juu ya kitabu cha "Mbinu za Kijeshi za Sunzi". Hivi sasa mawazo ya kitabu hicho yanatumiwa sana katika sekta nyingi zikwemo za kijamii na kibiashara.

Kitabu cha Historia

"Kitabu cha Historia" ni maandishi makubwa ya historia ya China, ni maandishi makubwa ya fasihi ya kuandika watu na mambo halisi, na kulikuwa na athari kubwa kwa elimu ya historia na fasihi kwa vizazi vilivyofuta vya China. "Kitabu cha Historia" kiliandikwa na Si Maqian katika enzi ya Han ya magharibi, karne ya kwanza kabla ya Kristu kuhusu mambo yaliyotokea katika miaka 3,000 iliyopita ya maeneo ya siasa, uchumi, utamaduni na historia tangu zamani za kale hadi enzi ya Han ya magharibi. Kitabu hicho alichoandika Si Maqian kwa miaka 13, kina makala 103 zenye maneno ya kichina zaidi ya laki 5, mambo aliyoandika ni pamoja na elimu ya sayari, kalenda, miradi ya maji, uchumi na utamaduni; shughuli na mambo kuhusu koo za kifalme na mabwenyenye za enzi mbalimbali; na mambo kuhusu watu mashuhuri wa enzi mbalimbali na historia ya makabila madogomadogo. "Kitabu cha Historia" kiliandika mambo halisi wala siyo kama vitabu vitatu walivyoandika maofisa wa historia wa enzi mbalimbali, ambavyo viliandika mafanikio tu na kusifu wafalme na mawaziri wao.


1 2 3 4 5 6