14: Historia

Mambo Makubwa Katika Historia

Vipindi Vitano Vyene Ustawi

Katika historia ndefu ya kimwinyi yenye miaka zaidi ya 2,000 vilitokea vipindi kadhaa vyenye ustawi, ambavyo ni pamoja na kipindi cha "Wenjing" cha enzi ya Han ya magharibi, kipindi cha "Zhenguan" cha enzi ya Tang, kipindi cha "Yongxuan" cha enzi ya Ming, kipindi cha "Kangyong" cha enzi ya Qing pamoja na kipindi ambacho watu wengi hawakijui cha "Zhangguo".

Kila kipindi chenye ustawi kina umaalumu wa namna moja, yaani sehemu zote zimeunganishwa kama kitu kimoja, uchumi unastawi, siasa vimetulia, jamii yenye amani na usalama, nguvu ya nchi imeimarika na utamaduni umeendelezwa vizuri.

Katika kipindi cha Chunqiu utaratibu ulivurugika, Confucius alikichukulia kuwa ni kipindi chenye vurugu, lakini mambo yalionesha kuwa utaratibu wa zamani utaangamia na utaratibu mpya utatokea. Baada ya kuingia kipindi cha Zhanguo, Lili na Wuqi walifanya mageuzi kwa mbalimbali katika nchi ya Wei na nchi ya Chu. Ilipofika miaka ya kati na mwisho ya kipindi hicho nchi za Qin, Han, Qi, Zhao na Yan ziliimarika kutokana na mageuzi, hususan ni kuwa Sangyang alifanya mageuzi makbuwa zaidi katika nchi ya Qin, hatimaye nguvu ya Qin ilikuwa kubwa zaidi kuliko nchi nyingine 6. Ingawa mageuzi yalifanywa kwa viwango tofauti katika nchi mbalimbali za kipindi kile, lakini hatimaye zilimaliza au kimsingi zilimaliza mageuzi ya utaratibu wa jamii, na utaratibu wa kitumwa ulibadilishwa na utaratibu wa kimwinyi.

Nchi ya Qin, ambayo iliteka nchi nyingine 6, ilitawaliwa kidikteta na mfalme mmoja, na ni mara ya kwanza kutimiza nadharia ya "mungano mkubwa" uliotarajiwa toka kipindi cha Chunqiu. Tokea hapo, mungano na mfarakano ilikuwa moja ya kanuni inayotumika kuangalia maendeleo ya jamii. Ni dhahiri kuwa aina zote za mungano ni sahihi na aina zote za mfarakano ni makosa. Wakati nchi fulani ikitawaliwa na ufisadi, maendeleo ya nguvu ya uzalishaji mali yamekwamishwa vibaya au kuzorota, wananchi wanaishi kwa shida kubwa, uasi wa wakulima ukafarakanisha umoja wa nchi hiyo, basi ufarakanishaji huo ni mzuri na unatakiwa kufanya hivyo. Hayati Mao Zedong kupongeza umuhimu wa uasi wa wakulima wa China ndiyo kutokana na msingi huo. Lakini baada ya mfarakano nchi kwa vyovyote itarejea katika mungano, hii ni kanuni ya maendeleo ya historia ya China, kwani muungano mkubwa unaleta mazingira tulivu ya jamii, ambayo yananufaisha maendeleo ya uzalishaji mali wa jamii na uboreshaji wa maisha ya wananchi. Katika wakati huo kutimiza "mungano mkubwa" ni sharti kubwa la kuangalia kipindi cha historia ni chenye ustawi ua la.

Enzi za Han na Tang, ambazo "muungano mkubwa", hivyo ni vipindi viwili muhimu vya historia, ambapo eneo la China lilipanuka.

Kila kipindi chenye ustawi kilikuwa na mazingira ya "muungano mkubwa", kuwa na amani na usalama, maendeleo ya uzalishaji mali, nafaka za kutosha na serikali kuwa na fedha nyingi. Mfalme Wu wa enzi ya Han alistawisha nchi kwa miaka zaidi ya 60, nchi ilikuwa salama na kuwa na fedha nyingi. Katika miaka ya mwanzo ya enzi ya Tang, kila ukoo ulikuwa na akiba ya nafaka kwa miaka kadhaa. Katika miaka ya wafalme wa Yong na Xuan ya enzi ya Ming, wananchi waliishi maisha ya neema na nchi ilikuwa na nguvu kubwa ya kifedha. Katika miaka ya mfalme Kangxi ya enzi ya Qing, nchi ilikuwa na akiba kubwa zaidi, katika miaka ya 50 tangu Kangxi kuwa mfalme wa Qing, kodi zilisamehewa kote nchini kwa wiki moja katika muda wa miaka 3, wakati baadhi ya mikoa ilisamehe au kupunguza kodi kila mwaka. Qianlong aliporithi ufalme, Qing ilikuwa na nguvu kubwa zaidi, mfalme alisamehe kodi kote nchi kwa mara nne.


1 2 3 4 5 6