15: Fasihi ya Kale

Washairi Wakubwa katika China na Kale

Mwandishi wa tamthilia Li Yu

Katika historia ya fasihi ya milenia kadhaa, walitokea washairi na waandishi wengi wa tamthilia na riwaya, Bw. Li Yu alikuwa mmojawapo.

Li Yu alizaliwa mwaka 1610 katika Enzi ya Ming. Katika miaka alipokuwa na umri wa miaka 30 ndipo mabadiliko ya enzi za kifalme yalipotokea. Enzi ya Qing ambayo ni enzi ya mwisho ya umwinyi nchini China iliiangamiza Enzi ya Ming, na kusababisha msukosuko wa jamii, msukosuko huo uliendelea kwa miongo kadhaa. Maisha ya Li Yu yalikuwa katika mazingira hayo hadi alipokufa mwaka 1680.

Li Yu alifundishwa na fikra za Confucius toka alipokuwa mtoto akitamani kufuata njia iliyochukuliwa na wasomi wengi wa zamani yaani kupata wadhifa kwa kufanikiwa katika mtihani. Lakini bahati mbaya alikutana na mazingira ya wasiwasi wa jamii, alishiriki kwenye mtihani mara kadhaa lakini mara zote alishindwa. Tokea hapo aliacha kabisa njia hiyo, alianzisha duka ili alijipatie kipato kwa kuwasaidia wengine kuandika makala, na akiwa na muda alitunga tamthilia.

Mafanikio makubwa maishani mwa Li Yu ni tamthilia na nadharia ya utungaji wa tamthilia. Maandishi ya tamthilia yaliyobaki ni kumi ikiwa ni pamoja na "Samaki Wayo" na "Mapenzi ya Phoenix". Tamthilia zake zote ni za kueleza mapenzi na kusifu matumaini ya wapenzi vijana, na kuponda mila ya ndoa iliyoamuliwa na wazazi. Tamthilia zake zinapendwa sana na watazamaji na hata ziliigwa katika nchi za kusini mashariki za Asia, hadi sasa tamthilia zake zinaendelea kuigizwa.

Li Yu licha ya kuwa mwandishi wa tamthilia, yeye pia ni mwananadharia wa utungaji tamthilia na mwandishi wa riwaya. Riwaya zake za "Tamthilia Isiyo na Sauti" na "Jumba la Ghorofa" zinajulikana sana. Katika riwaya zake alitetea usawa kati ya wanaume na wanawake.

Mwandishi Mkubwa wa Tamthilia Guan Hanqing

Katika Enzi ya Yuan, Guan Hanqing alikuwa mwandishi mkubwa wa tamthilia. Tamthilia yake ya kuhuzunisha "Theluji katika Majira ya Joto" imechezwa kwa miaka 700 tokea ilipotungwa, na ilitafsiriwa kwa lugha nyingi na kuenea duniani.

Guan Hanqing aliishi katika karne ya 13, Enzi ya Yuan, alikuwa mtu mwerevu, mcheshi na mwenye elimu pana. Kadhalika, alikuwa hodari wa kupiga kinanda, kucheza ngoma, kupiga filimbi na kuwinda. Guan Hanqing kwa miaka mingi aliishi kwenye mji mkuu na aliwahi kuwa mganga katika hospitali ya kifalme, lakini alikuwa hana hamu na kazi hiyo bali alipenda zaidi kutunga tamthilia.

Katika miaka aliyoishi, jamii katika Enzi ya Yuan ilikuwa ya wasiwasi, na utawala ulikuwa mbaya, migongano kati ya matabaka na kati ya makabila ilikuwa mikubwa, wananchi waliishi vibaya. Guan Hanqing aliwahurumia sana watu maskini, aliacha wadhifa wake alikwenda miongoni mwa watu maskini ili kuwaelewa maisha yao na kwa kutumia tamthilia zake alifichua ubovu wa jamii na kuonesha matumaini yake.

Kutokana na kuwa alielewa sana maisha ya makabwera na kufahamu lugha zao, alipata uwezo mkubwa wa kuandika tamthilia zake. Tamthilia zake ziliwalilia watu walionyanyaswa na kuonesha moyo wa kupambana na unyanyasaji huo.

Tamthilia "Theluji katika Majira ya Joto" ilieleza uonevu uliompata msichana Dou E. Tamthilia hiyo ilipendwa sana na watazamaji katika karne kadhaa zilizopita, na inasifiwa kuwa ni moja ya tamthilia kumi za kuhuzunisha za China ya kale.

Maishani mwake Guan Hanqing aliandika tamthilia 67, lakini zilizobaki mpaka sasa ziko 18 tu. Katika tamthilia zake alikuwa makini sana kuumba taswira ya wahusika na kuonesha hisia za moyoni. Kati ya waandishi wa tamthilia hakuna hata mmoja kama yeye aliyefanikiwa kuumba sura nyingi mahususi zilizo tofauti katika tamthilia.

Guan Hanqing anachukua nafasi muhimu katika historia ya tamthilia na fasihi ya China, anasifiwa kama ni "Shakespeare wa Mashariki".

1 2 3 4 5