23: Ala za Muziki

Kinanda cha Mdomo

Kouxuan

Kouxuan ni kinanda kidogo cha kutia mdomoni. Inasemekana kwamba kinanda hicho kilitokea katika karne ya 40 K.K.

Kinanda hicho kinatoa sauti kwa kugusa kipande chembamba kidogo, na sauti tofauti zinategemea idadi na unene wa vipande hivyo, kwa kawaida kinakuwa na vipande vitano.

Kwa kawaida vipande vyembamba hutengenezwa kwa shaba au chuma.

Anayepiga kinanda hicho anatumia kidole gumba na cha kati cha mkono wa kushoto kushika kinanda na kutia vipande kati ya midomo, na kutumia kidole gumba na cha kati cha mkono wa kulia kugusa vipande kutoa sauti. Ili kukuza sauti, midomo lazima itoke nje kama kununa na kubadilisha uwazi wa kinywa kugeuza mtindo wa sauti.


1 2 3 4 5 6 7