23: Ala za Muziki

Ala za Muziki kwa Mkwiro

Qing

Qing ina historia ndefu sana katika ala za muziki za kale, ni ala ya mawe na inatoa sauti kwa kugongwa.

Qing ilitumika sana katika zama za kale kwa ajili ya tambiko.

Kuna aina mbili za Qing, moja ni jiwe moja, nyingine ni mawe kadhaa. Qing ya jiwe moja inagongwa kwa ajili ya wafalme wanapofanya tambiko, na Qing yenye mawe mengi ni kwa ajili ya muziki katika kasri la kifalme.

Mwezi Agosti, mwaka 1978, kwenye kaburi la kale mkoani Hubei wataalamu wa mambo ya kale waligundua Qing, kengele mfululizo za muziki ambazo zimekuwa na miaka 2400. Jumla ya vipande 32 vya mawe ya Qing viligunduliwa. mwaka 1980 taasisi ya fizikia ya mkoa wa Hubei ilitengeneza vipande vya Qing kwa kuiga vya kale, sauti yake ilikuwa nzuri sana.

Mwaka 1983 kikundi cha nyimbo na dansi kilifanikiwa kutengeneza seti moja ya Qing yenye vipande vya mawe 32 ambayo inaweza kupiga muziki unaovutia sana.

Kengele Mfululizo za Muziki

Kengele hizo zinatundikwa kwenye fremu ya mbao na kila kengele inatoa sauti tofauti na nyingine.

Kengele hizo zilianza kuwepo kati ya Enzi ya Shang miaka 3500 iliyopita, lakini idadi ya kengele ilikuwa tatu tu, na idadi iliongezeka kutokana na jinsi jamii ilivyoendelea. Kengele za muziki zilitumika tu katika muziki wa kasri la kifalme au katika tambiko la wafalme.

Kengele zilizofukuliwa katika kaburi mkoani Hubei zilichongwa maneno 2800. kengele hizo ni hazina adimu na zinasifiwa kuwa ni ajabu katika historia ya utamaduni.

Mwaka 1982 kiwanda cha ala za muziki mjini Wuhan kilitengeneza seti moja ya kengele za muziki kwa kuiga kengele za kale, seti hiyo ina kengele 24 na kila kengele inaweza kutoa sauti mbili tofauti.

Muziki uliopigwa kwa kengele za kale unaonesha huzuni aliyokuwa nayo mshairi mkubwa Qu Yuan wa Dola la Chu.

Upatu

Upatu unatumika sana katika muziki wa Kichina na sherehe mbalimbali.

Upatu unatengenezwa kwa shaba, umbo lake ni la duara kama sahani, mpigaji anagonga kwa mkwiro.

Upatu uligunduliwa karne ya pili kusini magharibi mwa China. Katika vita vya zama za kale majemadari walikuwa hutumia upatu kuwatia moyo askari wao, na kuwaarishia warudi kwenye kambi zao.

Kuna aina 30 za upatu kutokana na ukubwa tofauti.

Upatu mkubwa una kipenyo sentimita 30 na hadi 100, unatumika katika muziki wa bendi kubwa.

Upatu mdogo una kiasi ya kipenyo sentimita 21 hadi 22.5, ni ala ya muziki inayotumika sana katika opera ya Kibeijing na opera nyingine za kienyeji.

Ngoma

Ngoma nchini China ina historia ya miaka 3000 hivi. Ngoma katika zama za kale ilikuwa ikitumika sana katika tambiko, ngoma, kufukuza wanyama na kuashiria hali ya hatari. Kutokana na jinsi jamii ilivyoendelea, matumizi ya ngoma yamekuwa mengi na kuanza kutumika katika muziki, opera, dansi na nyimbo, mashindano ya riadha na sherehe. Ngoma zina aina nyingi, licha ya kawaida, pia kuna ngoma ya kufungwa kiunoni, na ngoma yenye umbo la bakuli.

Ngoma ya kiunoni inawambwa kwa ngozi ya farasi, kwenye pande mbili za ngoma hiyo ndefu, kuna vishikizo vya kufunga kiunoni, ngoma hiyo hutumika katika ngoma ya kienyeji kaskazini mwa China.


1 2 3 4 5 6 7