24: Wanamuziki

Waongoza Muziki

Yan Liangkun

Mwongozaji wa bendi Bw. Yan Liangkun alikuwa naibu mwenyekiti wa jumuiya ya wanamuziki ya China, mratibu mkuu wa jumuiya ya waongozaji wa kwaya na mwongozaji wa benki ya taifa. Alizaliwa katika mji wa Wuhan mwaka 1923. Mwaka 1942 alisoma katika kitivo cha nadharia cha chuo cha muziki wa taifa, mwalimu wake wa muziki alikuwa profesa Jiang Dingxian na alijifunza uelekezaji wa bendi kwa kumfuata Bw. Wu Bochao. Mwaka 1947 alihitimu masomo yake na kwenda kufanya utafiti wa nadharia katika chuo cha muziki cha China mjini Hong Kong na kufundisha uongozaji wa bendi katika chuo hicho.

Baada ya China mpya kuasisiwa mwaka 1949, Bw. Yan Liangkun alifundisha muziki katika chuo cha muziki cha taifa na kuwa mwelekezaji wa bendi ya kwaya wa kikundi cha waimbaji vijana cha chuo hicho, na alikuwa mwongozaji wa kikundi cha kwaya cha taifa mwaka 1952. alikwenda Urusi kuchukua mafunzo mwaka 1954, aliporejea nchini mwaka 1958 alikuwa mwelekezaji wa kikundi cha kwaya cha taifa.

Mwaka 1983 kamati ya Kodaly ya Hungary ilimtunukia shahada na medali ya kumbukumbu kutokana na mchango aliotoa katika kuwafahamisha watu muziki na mafunzo ya Kodaly. Alishiriki kwenye matamasha mengi ya muziki. Mwaka 1986 aliteuliwa kuwa mjumbe wa kudumu katika tamasha la pili la kwaya mjini Beijing na kuwa kiongozi wa tamasha hilo. Kikundi cha kwaya cha taifa alichoongoza kilipata nafasi ya kwanza ya tuzo ya ngazi ya kwanza katika "tamasha la kwaya la Beijing."

Bw. Yan Liangkun aliongoza kikundi cha waimbaji kufanya maonesho na alialikwa kwenda kuongoza bendi Amerika ya kaskazini, Asia ya Kusini Mashariki, Taiwan na Hong Kong, na mara kwa mara alikwenda sehemu mbalimbali nchini kufundisha muziki. ?

Piao Dongsheng

Bw. Piao Dongsheng alizaliwa mwaka 1934 katika mji wa Shenyang mkoani Liaoning, tangu mwaka 1949 alifanya kazi za sanaa na alikwenda kusoma katika chuo cha fasihi na sanaa cha Lu Xun. Bw. Piao Dongsheng alikuwa mwelekezaji wa ngazi ya kwanza ya taifa wa kikundi cha nyimbo na ngoma cha taifa na kuwa kiongozi wa shirika la uchapishaji wa audio na video. Hivi sasa yeye ni kiongozi wa jumuiya ya muziki wa orchestral wa jadi ya taifa na mjumbe wa kamati ya uelekezaji wa wataalamu wa mtihani wa kiwango cha sanaa ya jamii ya wizara ya utamaduni.

Shughuli muhimu alizofanya Bw. Piao Dongsheng katika miaka zaidi ya miaka 50 iliyopita zilikuwa kuongoza bendi ya orchestral ya jadi. Aliwahi kuongoza bendi yenye wanamuziki elfu moja katika "maonesho makubwa ya China" ya tamasha ya kwanza ya sanaa ya China. Aliwahi kualikwa kufanya kazi za kuongoza bendi za ala za muziki za jadi ya Taibei, Gaoxiong, Hong Kong, Singapore, Chengdu na bendi ya ala za muziki za jadi ya kikundi cha nyimbo na ngoma cha taifa.

Licha ya kuelekeza bendi, vilevile alifanya kazi za kutunga muziki na utafiti wa nadharia ya muziki. Alitunga nyimbo karibu 100 ukiwemo "Muziki ya jadi ya Jiangsu", "kusherehekea ushindi" na "kwenye mbuga".

Mwaka 1993 aliteuliwa na wizara ya utamaduni ya China kuwa mtaalamu aliyetoa mchango mkubwa, na kupewa kiinua mgongo maalumu na serikali.

Hu Bingxu

Bw. Hu Bingxu ni mmoja wa waongozaji hodari wa bendi nchini China. Mwaka 1958 alishinda mtihani na kujifunza muziki wa orchestral katika chuo cha muziki cha taifa. Mwaka 1959 aliteuliwa kujifunza oboe katika darasa la wataalamu nchini Jamhuri ya Czech. Baada ya kumaliza masomo yake mwaka 1963 alikuwa mpiga oboe katika bendi ya symphony ya taifa.

Kwa nyakati mbalimbali Bw. Hu Bingxu alikuwa mwongozaji wa bendi na sanaa katika vikundi 7 vya ngazi ya taifa.

Aliwahi kushiriki maandalizi ya maonesho ya muziki wa symphony yakiwemo "Shajiabang" na "Mlima wa Cuckoo".

Kutokana na mafanikio aliyopata Bw. Hu Bingxu katika shughuli za uongozaji wa bandi alipewa tuzo na wizara ya utamaduni. Mwaka 1995 Bw. Hu Bingxu alipata tuzo maalumu ya "sahani ya dhahabu ya santuri".

Anaongoza bendi kwa ustadi na miondoko maridali, hususan yeye ni hodari sana kuhamasisha hisia za wanamuziki na maingiliano kati ya muziki na wasikilizaji. Sahani tatu zilizochapishwa mara ya kwanza na kampuni ya Philips katika China bara zilipigwa na bendi zilizoongozwa naye.

Bw. Hu Bingxu anazingatia kuendana na maonesho ya muziki na kuyapeleka katika mazingira mapya kabisa, na kuinua kiwango ustadi wa kuelekeza benki za ala za jadi katika kiwango cha ustadi wa uongozaji wa bendi wa kiwango cha juu duniani.

Mwaka 1999 aliongoza bendi ya ala za muziki za jadi ya taifa kufanya maonesho katika miji 18 ya Marekani na kufanya ushirikiano na mpiga fidla Ma Youyou ambaye ni mwanamuziki wa ngazi ya juu duniani, ambapo alipata mafanikio makubwa katika maonesho ya muziki uitwao "Ndoto ya Spring" yaliyofanywa katika ukumbi wa muziki wa Carnegie.

Chen Xiyang

Bw. Chen Xiyang alijifunza utungaji wa muziki mwaka 1960 katika chuo cha muziki. Alihitimu masomo kwa mafanikio mazuri mwaka 1965 na kuwa mwongozaji wa bendi ya orchestral ya kikundi cha ballet cha Shanghai. Tokea miaka ya 70 alifanya maonesho katika nchi nyingi zikiwemo Korea ya Kaskazini, Japan, Canada na Ufaransa.

Mwaka 1981 Bw. Chen Xiyang alijifunza uongozaji wa bendi katika Chuo Kikuu cha Yale cha Marekani, baada ya hapo alifanya ushirikiano na bendi za New York, Brooklyn na bendi ya Honolulu katika maonesho ya muziki.

Mwaka 1982 alialikwa kuongoza bendi katika tamasha la muziki ya Asbon, Marekani. Hapo baadaye alialikwa na kampuni ya sahani za santuri ya "Sauti ya Muziki" na kuongoza bendi ya symphony ya taifa ya Beijing kurekodi muziki ya mlango wa kwanza na wa nne wa Symphony ya Beethoven kwa ajili ya kutengenezesha sahani za santuri.

Toka mwaka 1985 Bw. Chen Xiyang alielekeza bendi ya kundi alilokuwa nalo au bendi za Urusi, Japan, Scotland, Italia, Uswisi, Hong Kong, Korea ya Kaskazini, Korea ya Kusini, Macao, Marekani, Thailand, Singapore, Australia na Ujerumani kufanya maonesho ya muziki huko.

Mwaka 1897 alipata tuzo ya uongozaji bora wa bendi katika tamasha ya muziki ya "Spring ya Shanghai" na muziki wa "Liangzhu" alioongoza ulipata tuzo ya sahani za dhahabu mwaka 1989. Jina lake liliorodheshwa katika "Orodha ya majina ya watu mashuhuri duniani" lililochapishwa na kituo cha takwimu za kimataifa cha Cambridge cha Uingereza.

Zheng Xiaoying

Profesa Zheng Xiaoying ni mwongozaji muziki wa kwanza wa kike nchini China. Alikuwa mwongozaji wa kwanza wa kundi cha opera la taifa na mkurugenzi wa kitivo cha uongozaji wa muziki cha chuo cha muziki cha taifa. Mwaka 1981 alipata tuzo ya ngazi ya kwanza ya uongozaji muziki na idara moja ya wizara ya utamaduni.

Mwaka 1947 alishinda mtihani wa kuingia chuo cha utibabu cha consonancy cha Beijing na kusomea elimu ya viumbe na muziki katika chuo cha wanawake cha Jinling. Mwaka 1948 alikwenda katika sehemu iliyokombolewa na kufanya kazi katika kikundi cha nyimbo na ngoma, mwaka 1952 alipelekwa kusomea utungaji wa muziki katika chuo cha muziki cha taifa. Mwaka 1955 alijifunza uelekezaji wa bendi na mwaka 1960 alikwenda kusoma nchini Urusi. Mwaka 1962 alifanikiwa kuelekeza bendi kupiga muziki wa opera ya Italia ijulikanayo kwa "Tosca" huko Moscow.

Tokea mwaka 1978 aliongoza bendi kufanya maonesho ya muziki ya kitaifa, ambapo aliongoza bendi kupiga muziki mwingi ya nchini na nchi za nje ikiwa ni pamoja na "bibi harusi wa mia moja", "The Fallen Woman" na "Carmen". Aidha, alishirikiana na bendi nyingi za nchini zikiwemo bendi ya muziki ya taifa, bendi ya symphony ya Shanghai, bendi ya symphony ya utangazaji na kundi la opera la taifa, muziki mwingi uliopigwa na bendi alizoongoza ulitengenezwa kuwa sahani za santuri.

Bibi Zheng Xiaoying ni mmoja wa profesa mwenye uzoefu mkubwa nchini katika eneo la uongozaji bendi za muziki. Wanafunzi wake kadhaa katika miaka ya karibuni walipata nafasi za mbele katika mashindano ya uelekezaji wa bendi ya kimataifa yakiwemo yale yaliyofanyika katika nchi za Marekani, Ufaransa, Italia, Austria, Jamhuri ya Czech na Ureno. Anapenda kueneza ufahamu wa elimu ya muziki kwa umma, na alifanya shughuli hizi mara karibu elfu moja, ambazo wasikilizaji wake wa moja kwa moja walikuwa zaidi ya laki mbili. Toka mwaka 1980 alifanya maonesho ya muziki zaidi ya 60 katika nchi za Japan, Marekani, Italia, Fenland, Ujerumani, Ufaransa, Uholanzi, Ubelgiji na Thailand, ambayo yalipendwa na watu wengi na kusifiwa na vyombo vya habari.

Li Delun

Bw. Li Delun ni mshauri wa bendi ya symphony ya China, naibu mwenyekiti wa jumuiya ya wanamuziki ya China. Mwaka 1917 alizaliwa katika Beijing, alijifunza upigaji wa piano na fidla alipokuwa mtoto, na aliposoma katika chuo kikuu cha Furen aliwashirikisha walimu na wanafunzi kuanzisha bendi ya orchestra na kufanya maonesho. Mwaka 1940 alifaulu mtihani wa kuingia chuo cha muziki cha taifa mjini Shanghai, akaanza kujifunza upigaji wa fidla kubwa kutoka kwa mwalimu Shevtzov na mwalimu R. duckson na kujifunza nadharia ya muziki kutoka kwa mwalimu W. Frankel.

Mwaka 1942 yeye na wenzake walianzisha "Bendi ya symphony ya vijana ya China". Baada ya kumaliza masomo yake katika chuo cha muziki mwaka 1943 alikwenda kufundisha na kufanya kazi ya uongozaji wa bendi katika Yanan. Na alikuwa mwongozaji wa bendi katika kikundi cha opera cha taifa mjini Beijing mwaka 1949.

Mbali na kufanya maonesho katika sehemu mbalimbali nchini Bw. Li Delun aliongoza bendi ya symphony ya taifa kufanya maonesho nchini Japan, Korea ya Kaskazini, Hong Kong na Macao, licha ya hayo aliongoza bendi ndogo kufanya maonesho katika miji zaidi ya 20 nchini Hispania. Aliwahi kualikwa kuongoza bendi zaidi ya 20 za nchi za nje zikiwemo za Leningrad, Moscow na za nchi za Finland, Czech na Cuba. Mwaka 1987 alielekeza bendi kubwa yenye wanamuziki 800 katika tamasha ya muziki ya "Spring ya symphony " yaliyofanyika mjini Beijing.

Baada ya mwaka 1985, Bw. Li Delun alikwenda kufanya maonesho ya muziki katika nchi za Luxembourg, Hispania, Ujerumani, Ureno, Canada na Marekani. Alielekeza bendi kupiga muziki iliyotungwa na wanamuziki mashuhuri zikiwemo "Kwaya ya mto Manjano" na "Wimbo wa misitu milimani". Aidha aliwahi kufanya maonesho kwa ushirikiano na wanamuziki mashuhuri wa duniani na nchini.

Mwaka 1985 Bw. Li delunhuko Paris aliteuliwa kuwa mjumbe wa kamati ya waamuzi ya mashindano ya upigaji fidla ya kimataifa, mwaka 1986 aliteuliwa kuwa mjumbe wa kamati ya waamuzi ya mashindano ya fidla kubwa ya kimataifa ya Tchaikovsky yaliyofanyika huko Moscow.

Katika miaka mingi iliyopita, Bw. Li Delun alishughulikia uenezaji na maendeleo ya muziki wa symphony , alianzisha bendi katika miji zaidi ya 20 nchini ikiwemo Beijing na Tianjin na kuziandalia mafunzo.

Mwaka 1980 Bw. Li Delun alipata tuzo ya uongozaji wa bendi ya wizara ya utamaduni. Mwaka 1986 alipata medali ya kumbukumbu ya Liszt kutoka wizara ya utamaduni ya Hungry. Alifariki dunia tarehe 19 mwezi Oktoba mwaka 2001 akiwa na umri wa miaka 84. )

Chen Zuohuang

Bw. Chen Zuohuang alizaliwa katika mji wa Shanghai, na alimaliza masomo yake ya uongozaji wa bendi mwaka 1981 katika chuo cha muziki cha taifa. Mwaka 1981 kutokana na mwaliko wa Bw. Seiji Ozawa alikwenda kusoma katika Tanglewood Music Centre na chuo cha muziki cha Michigan nchini Marekani, alipata shahada ya udaktari kwenye sanaa ya uongozaji bendi.

Tokea mwaka 1885 hadi mwaka 1987, Bw. Chen Zuohuang alikuwa naibu profesa wa uongozaji wa bendi katika chuo cha Kansas nchini Marekani, na alipata hadi ya udaktari. Mwaka 1987 Bw. Chen Zuohuang alikuwa mwongozaji wa bendi ya taifa, aliongoza bendi hiyo kufanya maonesho ya muziki katika miji 24 ya Marekani ikiwemo New York na Washington, ambapo walisifiwa na wasikilizaji na waongozaji wa bendi.

Kati ya mwaka 1990 na mwaka 2000 Bw. Chen Zuohuang alialikwa kuwa msimamizi mkuu na mwongozaji wa bendi ya The Witchita Symphony Orchestra. Kati ya mwaka 1992 na mwaka 1996 Bw. Chen alifanya kazi hiyo hiyo katika bendi ya Rhode Island Philharmonic Orchestra.

Bw. Chen Zuohuang alialikwa kuwa mwongozaji wa bendi katika nchi na sehemu zaidi ya 20 zikiwemo za The Zurich Tonhalle Orchestra na Vancouver Symphony Orchestra. Ustadi wa uongozaji bendi unasifiwa na wasikilizaji na waongozaji wa muziki kuwa mwanamuziki hodari sana.

Mwaka 1996 Bw. Chen Zuohuang aliacha kazi alizofanya katika nchi za nje na kurejea nchini. Alianzisha kundi la Symphony Orchestra ya China na kuwa msimamizi mkuu wa sanaa wa kundi hilo. Kundi hilo linafuata utaratibu wa maonesho ya majira ya muziki unaotekelezwa duniani, katika miaka michache iliyopita alialika wanamuziki hodari zaidi ya mia moja kufanya maonesho ya muziki nchini. Shughuli hizo zimechangia sana maendeleo ya muziki wa Symphony nchini.

Peng Xiuwen

Bw. Peng Xiuwen ni mwelekezaji wa bendi na mtungaji muziki (1931-1996) alizaliwa mkoani Wuhan, alikuwa mwanamuziki mkubwa wa ala za muziki za jadi na mwongozaji wa kwanza wa bendi ya ala za muziki ya utangazaji ya taifa.

Bw. Peng Xiuwen alijifunza upigaji wa zeze la jadi na gambusi. Alihitimu masomo katika shule maalumu ya biashara mwaka 1949 na alifanya kazi katika kituo cha Radio cha Chongqing mwaka 1950.

Mwaka 1952 Bw. Peng Xiuwen alihamishwa katika bendi ya ala za muziki ya jadi, katika mwaka uliofuata alikuwa mwongozaji wa bendi na mtunga muziki.

Mwaka 1957 katika tamasha ya 6 ya vijana ya kimataifa iliyofanyika mjini Moscow bendi aliyoongoza ilipata medali ya dhahabu.

Mwaka 1981 kutokana na mwaliko wa bendi ya ala za muziki za jadi ya Hong Kong Bw. Peng Xiuwen alikuwa mwongozaji wa bendi hiyo. Katika mwaka huo aliteuliwa kuwa kiongozi wa sanaa wa bendi ya ala za muziki ya idara ya utangazaji ya China. Mwaka 1983 Bw. Peng Xiuwen aliteuliwa kuwa kiongozi wa bendi ya ala za muziki za jadi ya utangazaji ya China.

"Kuunganisha hisia zake na muziki na kuonesha hisia kwa muziki" ni sifa yake katika uongozaji wa bendi. Kutokana na kuongozwa naye, bendi hiyo ilichukua nafasi ya kwanza katika upigaji wa muziki wa ala za jadi.

Bw. Peng Xiuwen alitoa mchango mkubwa katika shughuli za muziki wa jadi, idadi ya muziki aliourekebisha na kutunga ni kati ya 400 hadi 500 hivi ikiwemo "Kwenye maua na mbalamwezi kando ya mto majira ya Spring" na "Muziki wa ngoma ya kabila la wa-yao". Licha ya hayo alijaribu kupiga muziki mashuhuri wa nchi za nje kwa ala za muziki za kichina ikiwa ni pamoja na "ngoma ya Horo" na "Ruins of Athens" ya Beethoven".

Baada ya kuingia miaka ya 80 ya karne iliyopita, Bw. Peng Xiuwen alitunga muziki mwingi na maarufu wa ala za muziki za jadi. Bw. Peng Xiuwen alifariki kutokana na kuugua tarehe 28 mwezi Desemba mwaka 1996 mjini Beijing.


1 2 3 4 5