-
Tafadhali nipeleke kwenye Hospitali ya Zhongxin. Unapopanda taxi na kutaka kwenda hospitali unaweza kumwambia dereva na kusema: qing song wo qu zhong xin yi yuan.qing song wo: tafadhali nipeleke, qu: kwenda, zhong xin yi yuan: Hospitali ya Zhongxin.
-
Unaelewa namna ya kuelekea huko?
Zhi dao zen me zou ma? Zhi dao: elewa, jua. Zen me: namna. Zou: kwenda. Ma: kisaidizi cha neno kwa kuuliza.
-
Tafadhali usiendeshe gari kwa kasi.
Kama dereva anaendesha gari kwa kasi, unaweza kumwambia: qing nin kai man dian er. Qing: tafadhali, nin: wewe, kai: endesha, man dian er: polepole.
-
Haya egesha hapa mlangoni.
Jiu: kiunganishi cha neno. Ting: egesha gari. Zai Men kou: kwenye mlango. Ba: kisaidizi cha neno kwa kuomba.