-
Twende kutalii.
Kama unataka kumwalika mtu kwenda pamoja nawe kutalii, unaweza kumwambia: wo men qu lu xing ba. Wo men: sisi, qu: kwenda, lu xing: kutalii, ba: neno la kisaidizi.
-
Una mpango gani wikiendi hii.
Zhou mo you shen me ji hua? Zhou mo: wikiendi, you: kuna, shen me: nini, ji hua: mpango.
-
Tunataka kwenda kwenye ukuta mkuu kwa gari.
Wo men xiang kai che qu chang cheng wan wan. Chang cheng: ukuta mkuu, kai che: endesha gari, wan wan: tembeatembea
-
Tufunge safari saa ngapi?
Kama ukitaka kumwuliza rafiki yako "Tufunge safari saa ngapi?" unaweza kusema: za men shen me shi hou chu fa? Za men: sisi, shen me shi hou: saa ngapi, chu fa: kufunga safari.
-
Ni umbali gani kutoka hapa hadi kwenye sehemu nyingine ya vivutio?
Kama mkitembelea sehemu moja ya vivutio, na unataka kujua ni umbali gani kutoka pale hadi kwenye sehemu nyingine ya vivutio, unaweza kusema: xia yi ge jing dian hai you duo yuan. xia yi ge: sehemu inayofuata, jing dian: sehemu ya vivutio, hai you: bado kuna, duo yuan: umbali gani.
-
Mandhari ya sehemu hii ni nzuri sana.
Zhe er de feng jing tai mei le.
Zhe er: sehemu hii, feng jing: mandhari, tai mei le: nzuri sana.