somo 30 kuendesha gari kwa kutalii

 ongea na CRI
 

Kuanzia mwaka 2008, siku za mapumziko ya taifa zimeongezeka kuwa 11 nchini China, na wakati wa sikukuu za mwaka mpya wa jadi na sikukuu ya taifa watu wanaweza kupata siku tatu za mapumziko ama wanapumzika kwa wiki moja mfululizo baada ya kupangwa vizuri.
Wachina wanapenda kutalii nje ya nyumbani kwao, watu wa familia moja moja au marafiki kadhaa huwa wanapenda kwenda pamoja kutalii, na baadhi yao wanapenda kuendesha magari yao wenyewe kwenda kutalii nje ya nyumbani kwao, wengine wanakodi magari na kuyaendesha kwenda nje kutalii.
Hivi sasa nchini China kuna makampuni ya kukodisha magari, utaratibu ni rahisi sana. Watalii wakiweka dhamana ya vitambulisho wanakubaliwa kukodi magari.