somo 35 Kunyolewa nywele

 ongea na CRI
 

Nchini China shughuli za kushughulikia nywele zimeendelezwa sana, idara nyingi za kushughulikia nywele kuna mafundi wanaoweza kukusaidia kushughulikia nywele zako, pamoja na kukusaidia kuchagua mtindo wa kisasa wa nywele, kukufanyia kazi ya kuosha nywele, kukata nywele, kupaka rangi, kuzifanya nywele ziwe na mawimbi na kadhalika, mafundi na wahudumu wana uchangamfu mkubwa na wanafanya kazi vizuri. Kama unataka kupata fundi unaweza kupiga simu na kuagiza kabla ya wakati, ndani ya idara hizo pia unaweza kununua vitu vya kutunza nywele, lakini bei siyo ya chini; na baadhi ya idara pia zinaweza kutoa huduma ya usingaji wa sehemu ya kichwa na kukuwezesha uone raha.