-
Ukitaka kujua mtu mwingine anapenda zaidi filamu gani, unaweza kusema: 你最喜欢哪部电影?Unapenda zaidi filamu gani?
你 nǐ, wewe.
最 zuì , zaidi.
喜欢 xǐ huan, penda.
哪部 nǎ bù, gani.
电影 diàn yǐng, filamu.
-
Ukiona kuwa filamu moja ni ya kuvutia, unaweza kusema:它的情节很有趣。Hadithi ya filamu hiyo inafurahisha.
它的情节 tā de qíng jié, hadithi ya filamu hiyo.
很有趣 hěn yǒu qù, inafurahisha.
-
Tiketi za filamu hiyo zilinunuliwa vizuri.
这部电影的 zhè bù diàn yǐng de, za filamu hiyo.
票房 piào fáng, tiketi zilizonunuliwa.
不错 bú cuò, vizuri.
-
Ukitaka kujua filamu moja itaoneshwa saa ngapi, unaweza kuuliza: 请问电影几点开演?Tafadhali niambie, filamu itaoneshwa saa ngapi?
请问 qǐng wèn, tafadhali niambie.
电影 diàn yǐng, filamu.
几点 jǐ diǎn, saa ngapi.
开演 kāi yǎn, oneshwa.