Historia ya kuonesha filamu mjini Beijing ilianza mwaka 1902, hivi leo mjini Beijing kuna majumba mengi ya filamu, majumba hayo yanajengwa na kuwa na hali nzuri ya juu siku hadi siku. Mjini Beijing watazamaji wanaweza kutazama filamu za aina mbalimbali za kichina au za nchi za nje, ama za Hong Kong na Taiwan kutokana na wanavyopenda. Ili kuwavutia watazamaji wengi, majumba ya filamu yanafuata utaratibu wa kupunguza bei kila wiki, watazamaji pia wanaweza kununua kadi maalum ya kupata punguzo la bei za tiketi.