somo 62 Kutazama maonesho ya michezo ya sanaa

 ongea na CRI
 
  • Hivi sasa watu wengi wanaagiza tiketi kwenye mtandao wa internet. Ukifanya hivyo, unaweza kusema: 我是在网上订的。Niliagiza kwenye mtandao wa internet.
    我 wǒ, mimi.
    是 shì, ni.
    网上 wǎng shàng, kwenye mtandao wa internet.
    订 dìng, agiza.
    的 de, kisaidizi cha neno.
  • Sarakasi ni maonyesho ya kijadi ya kisanii nchini China, unaweza kusema: 中国杂技是世界一流的。Sarakasi ya China ni ya kiwango cha juu duniani.
    中国 zhōng guó, China.
    杂技 zá jì, sarakasi.
    是 shì, ni.
    世界 shì jiè, dunia.
    一流的 yī liú de, kiwango cha juu.
  • Kutazama maonesho ya wachezaji ni tofauti na kutazama maonesho kwenye televisheni. Unaweza kusema: 现场表演的效果完全不一样。Kutazama maonesho ya wachezaji kunavutia zaidi kuliko kutazama maonesho kwenye televisheni.
    现场表演的效果 xiàn chǎng biǎo yǎn de xiào guǒ, maonesho ya wachezaji.
    完全 wán quán, kabisa,.
    不一样 bù yí yàng, tofauti.
  • Ukitaka kupiga picha pamoja na mchezaji fulani, unaweza kusema: 我能跟您合个影吗?Naweza kupiga picha pamoja na wewe?
    我能 wǒ néng, naweza.
    跟您 gēn nín, pamoja na wewe.
    合个影 hé gè yǐng, kupiga picha pamoja.
    吗 ma, kisaidizi cha neno.