Watalii wakifika China huwa wanataka kutazama maonesho ya sarakasi za China. Sarakasi za China ni moja kati ya michezo ya sanaa ya jadi nchini China. Baada ya kuanzishwa kwa Jamhuri ya watu wa China, michezo ya sarakasi ya China yenye umaalum wa kipekee wa kichina inaendelezwa vizuri, wanasarakasi huenda nchi za nje kufanya maonesho, michezo ya sarakasi imekuwa daraja la mawasiliano ya utamaduni kati ya China na nchi za nje, na wasanii wa sarakasi wa China wamepata tuzo mara kwa mara katika mashindano ya michezo ya sarakasi ya kimataifa, China imekuwa nchi inayojulikana zaidi duniani kwa michezo yake ya sarakasi.