Kupanda milima ni mchezo mzuri wa kujenga mwili, ambao unaweza kuwasaidia watu kujiburudisha. Nchini China kuna mashabiki wengi wa mchezo wa kupanda milima, kila wikiendi au katika siku za mapumziko, marafiki na watu wanaofanya kazi katika idara moja hukubaliana kwenda pamoja kupanda milima. Kwa desturi za China, siku ya tarehe 9 ya mwezi wa 9 kwa kalenda ya kilimo ya China ni siku ya kupanda milima.