Tuzo maalumu: safari ya siku 7 mkoani Xinjiang pamoja na tiketi ya kwenda na kurudi. Tuzo ya nafasi ya kwanza: seti moja ya mapambo ya mezani, pamoja na kitamba kirefu kimoja, mito miwili ya viti, kifuniko kimoja cha kuwekea tishu, ambacho juu yake yamechorwa maua matatu ya rangi nyekundu ya chungwa, na kijani-manjano ya mtindo wa kikale wa China. Mapambo hayo yanaweza kuongeza mvuto wa mapambo ya nyumbani. Tuzo ya nafasi ya pili: seti moja ya vitu vizuri vya hariri vinavyoonesha hali ya furaha na baraka katika utamaduni wa jadi wa China, likiwemo daftari moja, vizulia vidogo vinne vya kuwekea vikombe na kimoja cha kuwekea bakuli. Tuzo ya nafasi ya tatu: seti moja ya vifaa vya ofisini, ikiwemo mouse moja iliyochorwa kwa maneno ya kale ya Kichina na picha ya msichana mchina wa zama za kale, kalamu moja iliyochorwa sura za wahusika wa Opera ya Beijing, ambavyo vinaonesha utamaduni wa jadi wa China. |