Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
Walinzi wa amani wa China walioko nchini Liberia 2007/08/09

China ni moja ya nchi wajumbe wa kudumu wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa. Tangu mwezi Januari mwaka 1992 hadi hivi sasa, China imetuma wanajeshi zaidi ya 6,000 kushiriki kwenye shughuli 15 za kulinda amani zinazoongozwa na Umoja wa Mataifa.Bw. Yu Changzhong ni daktari wa kijeshi wa China. Mwezi Februari mwaka jana alitumwa kwenda Liberia, kujiunga na kikosi cha wanajeshi wa China kinachotekeleza majukumu ya kulinda amani nchini humo. Daktari Yu alieleza hisia zake alipofahamishwa kuwa anaweza kushiriki kwenye shughuli za kulinda amani za Umoja wa Mataifa, akisema  "Wakati huo nilikuwa na furaha, lakini pia nilikuwa na wasiwasi kidogo."

 

 

 

Siku moja ya askari mzee Bw. Fan Daquan 2007/08/02

Kila asubuhi Saa 12 asubuhi, askari Fan Daquan na wenzake wanaanza mazoezi ya siku nzima. Wao ni askari wa kufanya utengenezaji wa maderaya ya idara moja ya jeshi la ukombozi wa umma la China, kila siku kabla ya kupata kifungua kinywa, wanafanya mazoezi ya mwili na gwaride, utaratibu huo haubadiliki hata kama kukiwa na upepo au mvua kubwa.Kazi ya askari hao wa jeshi la nchi kavu ni kukarabati na kuvitunza vifaru na amotkaa zote ili kuhakikisha vifaa hivyo vinaweza kuwasaidia askari kumaliza mazoezi yote na kutumika kwenye mapigano. Naibu mkurugenzi wa idara ya siasa ya kikosi hicho Bw. Zhao Xinjun alisema, Bw. Fan Daquan ana umri wa miaka 32 tu, lakini alijiunga na jeshi miaka 13 iliyopita, na yeye ni mmoja kati ya askari hodari wa kikosi hicho.

 

 

Wanajeshi wa China wako mstari wa mbele katika kukabiliana na hatari 2007/07/26
Katika nchi nyingi duniani, majeshi yanabeba majukumu ya ulinzi na kufanya uokoaji wakati wa maafa, hali kadhalika kwa jeshi la China. China ni moja ya nchi zinazokumbwa na maafa mengi ya kimaumbile duniani, jeshi la China linawajibika na uokoaji wakati wa maafa. Senior Colonel Tian Yixiang ni mkurugenzi wa ofisi ya kukabiliana na matukio ya dharura kwenye makao makuu ya general staff ya jeshi la ukombozi la umma la China. Alieleza kuwa tangu China mpya kuasisiwa mwaka 1949, karibu shughuli zote za kukabiliana na maafa zilishirikisha jeshi la China. Alisema  "Hususan kwenye mafuriko makubwa ya mwaka 1963 yaliyoikumba sehemu ya Huabei, tetemeko la ardhi la Xingtai mwaka 1966 na tetemeko kubwa la ardhi lililotokea miaka 10 iliyofuata huko Tangshan, moto kubwa uliowashwa milimani Daxinganling mwaka 1987 na mafuriko makubwa yaliyozikumba sehemu nyingi za China mwishoni mwa miaka ya 1990. Kila mara yalipotokea maafa makubwa ya kimaumbile, kwa uhakika jeshi la China lilishiriki kwenye shughuli za kukabiliana na maafa. Hili ni jukumu la jeshi."
Jeshi la China lafanya juhudi katika ushirikiano wa kimataifa wa mapambano dhidi ya ugaidi 2007/07/25

 

Tarehe 1 Agosti mwaka huu itakuwa siku ya maadhimisho ya miaka 80 tangu liundwe jeshi la ukombozi wa umma la China. Na kuanzia tarehe 9 hadi 17 Agosti, luteka ya pamoja ya mapambano dhidi ya ugaidi ya "Jukumu la amani la mwaka 2007" itakayofanywa na majeshi ya nchi wanachama wa Jumuiya ya ushirikiano ya Shanghai itafanyika nchini China na Russia.Katika miaka ya hivi karibuni, jeshi la China limekuwa linafanya juhudi katika ushirikiano wa kimataifa wa mapambano dhidi ya ugaidi, na kusifiwa vilivyo na jumuiya ya kimataifa. Wiki iliyopita huko Guangzhou, China, vikosi maalum vya nchi kavu vya China na Thailand vilifanya luteka ya pamoja ya kijeshi kwa ajili ya kukabiliana na tishio la ugaidi.

 

China yaadhimisha miaka 80 ya jeshi la ukombozi wa umma la China  2007/07/24

Ili kuadhimisha kutimia kwa miaka 80 tangu kuundwa kwa jeshi la ukombozi wa umma la China, maonesho makubwa yenye eneo la mita za mraba 6,500 kuhusu historia ya ujenzi na maendeleo ya jeshi la China yamefunguliwa tarehe 16 mwezi Julai hapa Beijing. Kauli-mbiu ya maonesho hayo ni "Jeshi letu linaelekea kwenye jua?maendeleo ya ujenzi wa ulinzi wa taifa na jeshi". Kwenye sherehe ya ufunguzi iliyofanyika tarehe 16, mjumbe wa idara ya siasa ya kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha China ambaye pia ni mkuu wa idara ya uenezi ya kamati kuu ya chama Bw. Liu Yunshan alisema, jeshi la ukombozi wa umma la China liliundwa mwaka 1927, katika muda wa miaka 80 iliyopita, hususan baada ya kuasisiwa kwa China mpya mwaka 1949, maendeleo muhimu yamepatikana katika ujenzi wa kisasa wa ulinzi wa taifa na jeshi. 

Vikosi vya upande wa China vyaanza kukaa kwenye Kijiji cha makambi ya Luteka ya pamoja ya "Jukumu la amani la mwaka 2007" Viongozi wa kamati kuu ya kijeshi ya China na wajumbe wa mashujaa na hodari wa kuigwa wa jeshi la China washerehekea pamoja maadhimisho ya miaka 80 ya Jeshi la ukombozi wa umma la China
Vikosi vya jeshi la ukombozi wa umma la China vilivyoko Hongkong na Makau vyasherehekea miaka 80 ya Jeshi la China Makao makuu ya upande wa China ya jeshi litakaloshiriki kwenye luteka ya pamoja ya "Jukumu la Amani-2007" yafanya maandalizi
Gazeti la Renminribao la China latoa makala ya maadhimisho ya miaka 80 tangu kuanzishwa kwa jeshi la ukombozi wa umma wa China Mkutano wa maadhimisho ya miaka 80 ya Jeshi la ukombozi wa umma la China wafanyika Beijing
Ofisi za ubalozi wa China katika nchi za nje zafanya tafrija za kuadhimisha miaka 80 ya Jeshi la ukombozi wa umma la China Wizara ya ulinzi ya China yafanya tafrija ya kuadhimisha miaka 80 tangu kuundwa kwa jeshi la ukombozi wa watu la China
Jeshi la China laanza kupeleka askari kwenye luteka ya kimataifa kwa njia ya ndege Tamasha la kuadhimisha miaka 80 ya jeshi la ukombozi wa umma la China lafanyika hapa Beijing