Wizara ya ulinzi ya China tarehe 31 hapa Beijing imefanya tafrija, ili kuadhimisha miaka 80 tangu jeshi la ukombozi wa watu la China liundwe. Waziri wa ulinzi wa China Bw. Cao Gangchuan amehutubia tafrija hiyo akisema, jeshi la China linapenda kuongeza mawasiliano na ushirikiano na majeshi ya nchi nyingine duniani, na kutoa mchango mpya kwa ajili ya kulinda amani duniani.
Viongozi wa chama na serikali wa China wakiwemo rais Hu Jintao, spika wa bunge la umma Bw. Wu Bangguo na waziri mkuu Bw. Wen Jiabao wamehudhuria tafrija hiyo.
Bw. Cao Gangchuan ameeleza kuwa China itashikilia njia ya amani ya kujiendeleza, na kutekeleza sera ya kidiplomasia ya amani ya kujitawala na kujiamulia mambo na sera ya kujilinda, na inajitahidi kushirikiana na watu wa nchi nyingine duniani, ili kuhimiza kuijenga dunia iwe na amani ya kudumu, ustawi wa pamoja na masikilizano.
|