Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-07-24 16:55:02    
China yaadhimisha miaka 80 ya jeshi la ukombozi wa umma la China

cri

Ili kuadhimisha kutimia kwa miaka 80 tangu kuundwa kwa jeshi la ukombozi wa umma la China, maonesho makubwa yenye eneo la mita za mraba 6,500 kuhusu historia ya ujenzi na maendeleo ya jeshi la China yamefunguliwa tarehe 16 mwezi Julai hapa Beijing. Kauli-mbiu ya maonesho hayo ni "Jeshi letu linaelekea kwenye jua?maendeleo ya ujenzi wa ulinzi wa taifa na jeshi".

Kwenye sherehe ya ufunguzi iliyofanyika tarehe 16, mjumbe wa idara ya siasa ya kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha China ambaye pia ni mkuu wa idara ya uenezi ya kamati kuu ya chama Bw. Liu Yunshan alisema, jeshi la ukombozi wa umma la China liliundwa mwaka 1927, katika muda wa miaka 80 iliyopita, hususan baada ya kuasisiwa kwa China mpya mwaka 1949, maendeleo muhimu yamepatikana katika ujenzi wa kisasa wa ulinzi wa taifa na jeshi. Lengo la kufanya maonesho hayo ni kuonesha maendeleo ya ujenzi wa ulinzi wa taifa na jeshi la China, jeshi la China kutekeleza majukumu kwa uaminifu pamoja na mchango wake muhimu liliotoa katika kulinda na kujenga taifa.

"Uasi wa Nanchang wa kupinga udikteta wa chama cha Kuomintang cha China uliofanywa miaka 80 iliyopita, ulimaanisha kuwa chama cha kikomunisti cha China kilianza kuunda jeshi lake la mapinduzi, na kubeba jukumu la kihistoria la kuongoza mapigano ya kisilaha. Tokea hapo jeshi la umma likiongozwa na chama cha kikomunisti cha China, lilishiriki kwenye vita ya mapinduzi ya ardhi, vita ya kupambana na mashambulizi ya Japan na vita ya ukombozi, na lilitoa mchango mkubwa wa kihistoria kwa ajili ya uhuru wa taifa na ukombozi wa umma."

Bw. Liu Yunshan alisema tangu kuasisiwa kwa China mpya, jeshi la umma lilirithi desturi nzuri, kukuza moyo wa kimapinduzi, kulinda uhuru na mamlaka ya taifa, kuunga mkono ujenzi wa kisasa na kutoa mchango mkubwa kwa ajili ya ujenzi wa kiujamaa na utekelezaji wa sera za mageuzi na ufunguaji mlango. Historia ya miaka hiyo 80 inaonesha vilivyo kuwa, jeshi la ukombozi la umma ni jeshi tukufu linalotii chama, wananchi na taifa, na ni jeshi linaloshinda daima.

Maonesho hayo ni makubwa yenye mambo mengi, yanaonesha picha karibu elfu 1 na vitu zaidi ya 1,700, ambavyo vingi ni vyenye thamani kubwa na havikuoneshwa kwa watu, licha ya hayo zinaoneshwa zana na silaha za kisasa zinazotumiwa na jeshi la China. Mkuu wa jumba la makumbusho la mambo ya kijeshi ya mapinduzi ya umma la China, meja jenarali Guo Dehe alisema,

"Katika maonesho hayo inaoneshwa mifuko ya mchanga iliyotumika katika mashindano ya kijeshi yaliyofanyika katika miaka ya 50 ya karne iliyopita, ambayo Mao Zedong aliangalia, karatasi ya hotuba iliyoandikwa na Zhou Enlai wakati wa kupiga mizinga kwenye kisiwa cha Jinmen, kikokotoleo cha muundo wa kizamani kilichotumika wakati wa kufanya utafiti wa mabomu ya atomiki, bendera za taifa na za jeshi zilizopandishwa mara ya kwanza na vikosi vilivyoko Hong Kong na Macao, aidha, zinaoneshwa silaha nyepesi za kisasa za milimita 5.8, vifaru muhimu vya muundo wa kisasa, pamoja na silaha kubwa yakiwemo magari ya kivita, mizinga na makombora ya kupiga shabaha za ardhini."

Maonesho hayo licha ya kusamehe kiingilio kwa watazamaji, pia yana mambo mengi yanayoruhusu watazamaji kushiriki, ukiwemo mfumo wa mafunzo wa kuigiza manowari, ambapo watazamaji wanapata uzoefu wa kuendesha vifaru na manowari. Mwelezaji mmoja aliwaelekeza watazamaji namna ya kuviendesha alisema, "Manowari zinayumbayumba sana katika upepo na mawimbi makubwa. Mara onyo la vita likatolewa, ndege ya adui ikaonekana, hapo manowari zinapiga makombora na kupata shabaha, na ndege ya adui ikaangushwa chini."

Maonesho hayo yatafanyika kwa muda wa zaidi ya mwezi mmoja.

Idhaa ya kiswahili