Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-07-25 15:46:49    

Jeshi la China lafanya juhudi katika ushirikiano wa kimataifa wa

mapambano dhidi ya ugaidi

 


cri

Tarehe 1 Agosti mwaka huu itakuwa siku ya maadhimisho ya miaka 80 tangu liundwe jeshi la ukombozi wa umma la China. Na kuanzia tarehe 9 hadi 17 Agosti, luteka ya pamoja ya mapambano dhidi ya ugaidi ya "Jukumu la amani la mwaka 2007" itakayofanywa na majeshi ya nchi wanachama wa Jumuiya ya ushirikiano ya Shanghai itafanyika nchini China na Russia.

Katika miaka ya hivi karibuni, jeshi la China limekuwa linafanya juhudi katika ushirikiano wa kimataifa wa mapambano dhidi ya ugaidi, na kusifiwa vilivyo na jumuiya ya kimataifa. Wiki iliyopita huko Guangzhou, China, vikosi maalum vya nchi kavu vya China na Thailand vilifanya luteka ya pamoja ya kijeshi kwa ajili ya kukabiliana na tishio la ugaidi. Na luteka ya pamoja ya mapambano dhidi ya ugaidi ya "Jukumu la amani la mwaka 2007" ni luteka kubwa kabisa ya pamoja itakayofanywa na nchi wanachama wa Jumuiya ya ushirikiano ya Shanghai tangu jumuiya hiyo ianzishwe, na hii ni mara kwa kwanza kwa vikosi vya aina mbalimbali vyenye askari wengi kwenda nchi ya nje kushiriki kwenye luteka ya pamoja. Mtafiti wa chuo cha sayansi ya mambo ya kijeshi cha jeshi la ukombozi wa umma la China Bwana Zheng Shouhua alipohojiwa na mwandishi wetu wa habari alisema, jeshi la China litafanya ushirikiano kwa kina zaidi na majeshi ya nchi za nje kutokana na hali halisi. Akisema:

Zamani jeshi la China lilifanya ushirikiano na majeshi ya nchi za nje katika mapambano dhidi ya ugaidi, hasa kuhusu kuongeza maelewano na mawasiliano kati ya pande mbili mbili au pande nyingi, na kujenga utaratibu wa mawasiliano. Na katika siku zijazo jeshi la China na majeshi ya nchi za nje yatapanua maingiliano katika upelelezi, uongozaji, utekelezaji wa mipango, teknolojia na nadharia, ambapo yataongeza mambo ya mawasiliano, tena jeshi la China litafanya ushirikiano na majeshi ya nchi nyingi zaidi.

Mtaalamu huyo wa kijeshi anaona kuwa, serikali ya China na jeshi la China kufanya juhudi katika ushirikiano wa kimataifa wa mapambano dhidi ya ugaidi, na kuonesha umuhimu wake mkubwa katika kupambana na ugaidi duniani. Kwa mfano jeshi la China lilionesha umuhimu wake katika kampeni ya kufunga na kudhibiti mipaka wakati wa vita vya Afghanistan, na kupashana habari za upelelezi na nchi majirani kuhusu mapambano dhidi ya ugaidi. Hasa tokea mwaka 2002, jeshi la China lilifanya luteka ya pamoja ya mapambano dhidi ya ugaidi ya pande mbili mbili au pande nyingi na nchi za Kyrgyzstan, Jumuiya ya ushirikiano ya Shanghai, Russia, Pakistan, Tajikistan na nyinginezo, luteka hizo zimeonesha umuhimu katika kupambana na jumuiya za kigaidi na kuzuia shughuli za kigaidi.

Lakini Bwana Zheng Shohua amedhihirisha pia kuwa, luteka zilizofanywa na jeshi la China na majeshi ya nchi nyingine katika siku zilizopita, nyingi zilikuwa luteka ndogo zilizowashirikisha wanajeshi wachache, ambapo mazoezi ya kijeshi yaliyohusishwa yalikuwa ni machache sana, na hasa yalikuwa ni kwa ajili ya kutafuta njia na kuongeza uzoefu. Katika siku zijazo, luteka hizo zitafanyika kwa kina zaidi, ambapo zitafanyika kwa kuelekea hali halisi ya kimapigano, na njia za mazoezi pia yatafanyika kwa unyumbufu zaidi ili kupata ufanisi zaidi. Alisema

"Kutokana na maendeleo ya kina ya ushirikiano, pande mbili mbili au pande nyingi za ushirikiano zitafanya utafiti kuhusu namna ya kutatua matatizo kadhaa halisi ili kupata ufanisi halisi katika ushirikiano wa mapambano dhidi ya ugaidi."

Bwana Zheng Shouhua alisema, kuna haja ya lazima kuimarisha ushirikiano wa kimataifa na kikanda katika mapambano dhidi ya ugaidi, hasa kufanya ushirikiano na nchi majirani katika mapambano dhidi ya ugaidi. Alisema:

"Kama tutajenga utaratibu mzuri wa kupashana habari za upelelezi na jumuiya ya kimataifa, ndipo tutakapoweza kujua mwelekeo wa shughuli za kigaidi, na kama tunachukua hatua za pamoja na jumuiya ya kimataifa hasa majeshi ya nchi jirani, ndipo tutakapoweza kupambana pamoja na shughuli za ugaidi, na kuweka mfumo mkubwa wa mapambano dhidi ya ugaidi kote duniani au kwenye sehemu, basi magaidi watapigwa pigo kali bila kujali watakakokwenda".

Idhaa ya kiswahili 2007-07-22