Matumizi ya majumba na viwanja vya Michezo ya Olimpiki ya Beijing yahimiza wananchi wa China kujenga mwili 2008-10-24 Karibu kila baada ya Michezo ya Olimpiki, miji wenyeji ilikabiliana na matatizo ya uendeshaji wa majumba na viwanja vya michezo, hata baadhi ya miji wenyeji ilibeba mizigo mikubwa ya kiuchumi kutokana na gharama kubwa za ujenzi wa majumba na viwanja hivyo. |
Napenda Beijing! 2008-10-10 Balozi wa China nchini Marekani Bw. Zhou Wenzhong hivi karibuni alifanya tafrija kubwa ya kupongeza mafanikio ya Michezo ya Olimpiki ya Beijing ya mwaka 2008, na kushukuru uungaji mkono mkubwa na ushirikiano wa watu wa sekta mbalimbali wa Marekani kwa China katika kuiandaa Michezo ya Olimpiki. Watu walioalikwa kwenye tafrija hiyo walieleza kuwa, Michezo ya Olimpiki ya Beijing si kama tu ni michezo mikubwa, bali ni shughuli kubwa zaidi za mawasiliano ya utamaduni kati ya China na dunia, na kuwafanya watu wengi zaidi kuifahamu China.
|
Mashindano ya kupiga makasia yawavutia wachina kufuatilia mchezo wa mashua yenye matanga 2008-03-18 Ikilinganishwa na nchi za Ulaya na Marekani, mchezo wa mashua zenye matanga nchini China ulichelewa kuanza. Hivi sasa Michezo ya Olimpiki ya Beijing ya mwaka 2008 inakaribia, ukiwa mji utakaoaandaa mashindano ya mashua zenye matanga wakati wa Michezo ya Olimpiki, Qingdao imeanza kuwahimiza watu wengi zaidi washiriki kwenye mchezo huo. |
Madereva wa Taxi wa Beijing wafanya juhudi za kufanya maandalizi ili kutoa huduma bora wakati wa Michezo ya Olimpiki ya Beijing 2008-03-11 Wakati Michezo ya Olimpiki ya Beijing inapokaribia, watu wa sekta mbalimbali wanafanya juhudi kubwa kwa ajili ya maandalizi ya michezo hiyo, ikiwa ni pamoja na madereva wa taxi ambayo ni moja ya njia muhimu za mawasiliano kwa wakazi wa Beijing. Ili kuwakaribisha wageni kutoka nchi mbalimbali duniani wakati wa Michezo ya Olimpiki, madereva wa taxi wanafanya juhudi kubwa ili waweze kutoa huduma bora wakati wa michezo hiyo. |
Timu ya soka ya wanawake ya China yajipima kwa kupitia mashindano ya soka ya Asia Mashariki 2008-03-04 Mashindano ya pili ya soka ya Asia Mashariki yalifanyika mwezi Februari kwenye miji ya Chongqing na Yongchuan, kusini magharibi nchini China. Mashindano hayo yalizishirikisha timu nne zenye uwezo mkubwa duniani zikiwa ni pamoja na timu za Japan, Korea ya Kusini, Korea ya Kaskazini na China. Kabla ya Michezo ya Olimpiki ya Beijing, timu ya soka ya wanawake ya China ilikuwa ina matumaini ya kujipima uwezo wake kwa kupitia mashindano yenye kiwango cha juu kama hayo, ili kupata maendeleo mapya. |
Kushindwa kwawasaidia wachezaji wa kuteleza barafu wa China kupata maendeleo mapya 2008-02-26 Michezo ya 11 ya majira ya baridi ya China ilimalizika hivi karibuni katika miji ya Qiqiha'er na Harbin nchini China. Kwenye mashindano ya kuteleza kwenye barafu kwa mitindo mbalimbali, mabingwa wa mchezo wa kuteleza kwenye barafu kwa wachezaji wawili wawili duniani Pang Qing na Tong Jian walipata medali ya dhahabu na fedha katika michezo ya Short Program na kuteleza kwenye barafu kisanii. Mafanikio hayo yana umuhimu mkubwa kwa wachezaji hao wawili, kwani yalipatikana kutokana na juhudi kubwa. |
Beijing inavyofanya juhudi za kutoa mafunzo kwa ajili ya Michezo ya Olimpiki ya Walemavu 2008-02-19 Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya mwaka 2008 itafunguliwa baada ya nusu mwaka mjini Beijing, China. Kila Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ni tamasha kubwa kwa walemavu duniani, na michezo hiyo itakayofanyika nchini China itakuwa fursa nzuri kwa maendeleo ya shughuli za walemavu nchini China. Ili kuiandaa michezo hiyo kwa mafanikio, Beijing inafanya maandalizi kwa juhudi kubwa, na kuanzisha kazi ya kutoa mafunzo kwa pande zote. |
China yapambana na matumizi ya dawa za kuongeza nguvu 2008-02-12 Dawa za kuongeza nguvu ni tatizo kubwa linaloikabili michezo mbalimbali duniani. Wakati Michezo ya Olimpiki ya Beijing inapokaribia, China ikiwa nchi mwenyeji ya michezo hiyo, kazi yake katika kupambana na dawa za kulevya inafuatiliwa sana. Kuanzia mwishoni mwa miaka ya 80 ya karne iliyopita, wachina waligundua hatari zinazosababishwa na matumizi ya dawa za kuongeza nguvu, na katika miaka 20 iliyopita wamekuwa wakipinga matumizi ya dawa hizo. |
Mkakati wa maendeleo ya muda mrefu wa michezo ya majira ya baridi ya China wapata maendeleo mazuri 2008-02-05 Michezo ya 11 ya Majira ya Baridi ya China ilifanyika mwezi Januari mkoani Heilongjiang nchini China. Mkurugenzi wa Kituo cha usimamizi wa michezo ya majira ya baridi ya Idara kuu ya Michezo ya taifa ya China ameeleza kuwa, michezo ya kuteleza theluji kwa kutumia ubao kwa mwanamume kwenye uwanja wenye umbo wa U, na kuteleza kwenye barafu kwa vitendo mbalimbali imepata maendeleo mazuri katika miaka ya hivi karibuni, hali ambayo imeonesha kuwa mkakati wa maendeleo ya muda mrefu wa Michezo ya majira ya baridi ya China umepata maendeleo dhahiri. |
Timu ya riadha ya China yajiandaa kwa ajili ya Michezo ya Olimpiki ya Beijing 2008-01-29 Ili kujiandaa kwa ajili ya Michezo ya Olimpiki ya Beijing ya mwaka 2008, timu ya riadha ya China imeanza kufanya mazoezi katika majira ya baridi, na hiki ni kipindi muhimu kwa timu ya China kuongeza uwezo wake. Mwaka 2007 timu ya riadha ya China ilipata mafanikio mbalimbali. Kwenye Mashindano ya riadha duniani yaliyofanyika huko Osaka, timu ya China ilipata medali moja ya dhahabu, moja ya fedha na moja ya shaba, na kushika nafasi ya 11 kwenye orodha ya medali, na hayo ni mafanikio makubwa zaidi iliyopata timu ya China tokea Mashindano ya riadha duniani yaliyofanyika huko Monte Carlo mwaka 1993; Kwenye mashindano ya riadha ya Asia, timu ya China ilipata medali saba za dhahabu, tano za fedha na nne za shaba, na kushika nafasi ya kwanza tena barani Asia. |
|