Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-02-05 16:35:43    
Mkakati wa maendeleo ya muda mrefu wa michezo ya majira ya baridi ya China wapata maendeleo mazuri

cri
Michezo ya 11 ya Majira ya Baridi ya China ilifanyika mwezi Januari mkoani Heilongjiang nchini China. Mkurugenzi wa Kituo cha usimamizi wa michezo ya majira ya baridi ya Idara kuu ya Michezo ya taifa ya China ameeleza kuwa, michezo ya kuteleza theluji kwa kutumia ubao kwa mwanamume kwenye uwanja wenye umbo wa U, na kuteleza kwenye barafu kwa vitendo mbalimbali imepata maendeleo mazuri katika miaka ya hivi karibuni, hali ambayo imeonesha kuwa mkakati wa maendeleo ya muda mrefu wa Michezo ya majira ya baridi ya China umepata maendeleo dhahiri.

Ili kuhimiza maendeleo ya michezo ya majira ya baridi ya China, Idara kuu ya Michezo ya China imeweka mkakati wa maendeleo ya muda mrefu wa miradi ya majira ya baridi ya China ili kuhimiza michezo ya majira ya bariki ipate maendeleo mapya.

Kutokana na hali ya hewa, zamani michezo ya majira ya baridi iliweza tu kufanyika kwenye sehemu za Kaskazini-Mashariki nchini China ambazo hali ya hewa ya huko ni ya chini wakati wa majira ya baridi, lakini hivi sasa viwanja vya barafu na theluji vimejengwa katika miji ya kusini nchini China ikiwemo Shanghai na Shenzhen, na hayo ni mafanikio makubwa yaliyopatikana kutokana na Mkakati wa maendeleo ya muda mrefu ya Michezo ya Majira ya Baridi ya China. Kwa kuwa michezo ya majira ya baridi inaathiriwa na hali ya hewa, maendeleo ya michezo hiyo yanahitaji gharama kubwa, na haiwezi kupatikana kwa kutumia fedha zinazotengwa na serikali tu, hali ambayo inauhimiza uendeshaji wa soko iwe njia muhimu ya kuhimiza michezo hiyo. Bw. Wang Yitao alisema:

"Serikali imetangaza sera za kuhimiza michezo hiyo ianzishwe kwenye mikoa yenye mazingira mazuri. Hivi sasa viwanja vya barafu na theluji vinajengwa kutokana na fedha zinazotolewa na viwanda na serikali. Maendeleo ya mchezo wa barafu na theluji yanatokana na maendeleo ya jamii ya nchi."

Ili kuhimiza maendeleo yenye uwiano kati ya Michezo ya kiangazi na majira ya baridi, hususan kuzifanya sehemu za kusini za China ziweke mkazo katika michezo ya majira ya baridi, Idara kuu ya michezo ya China iliongeza michezo 14 ya majira ya baridi kwenye Michezo ya 10 ya taifa la China. Bw. Wang Yitao amedokeza kuwa, michezo minne ya majira ya baridi itaongezwa kwenye michezo hiyo ya 11, na sehemu mbalimbali za China zitafuatilia zaidi michezo ya majira ya baridi.

Kuhimiza maendeleo yenye uwiano kati ya michezo ya barafu na theluji ni kazi nyingine muhimu kwa mchezo wa majira ya baridi wa China. Hivi sasa wachezaji wa China wana uwezo wa kugombea medali za dhahabu kwenye michezo sita katika Michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi, ikiwa ni pamoja na mchezo wa mbio za mita 500 za kuteleza barafu kwa wanawake, mbio za mita 1000 kwa wanawake, mbio za kupokezana kwa kutekelza barafu kwa wanawake, kuteleza barafu kwa mtindo mbalimbali kwa wachezaji wawili wawili na ustadi angani wakati wa kuteleza theluji kwa wanaume na wanawake. Kati ya michezo hiyo sita kuna michezo miwili tu ya theluji, hali ambayo imeonesha kuwa kiwango cha theluji kiko nyuma cha mchezo wa barafu. Kutokana na hali hiyo, kituo cha usimamizi wa michezo ya majira ya baridi ya Idara kuu ya Michezo ya taifa ya China imetilia maanani katika mchezo wa kuteleza theluji kwa ubao kwenye uwanja wenye umbo wa U, na wachezaji wa mchezo huo wameshika nafasi ya tano na nafasi ya pili kwenye Mashindano ya dunia na Mashindano ya kombe la dunia.

Mkakati wa maendeleo ya muda mrefu kwa michezo ya majira ya baridi ya China pia umeweka malengo katika namna ya kuinua kiwango cha michezo ya barafu ambayo ina sifa katika muda mrefu uliopita. Akizungumzia mchezo Ice Ballet, naibu mkurugenzi wa Kituo cha usimamizi wa michezo ya majira ya baridi kwenye Idara kuu ya Michezo ya taifa ya China Bw. Ren Hongguo amesema, kikilinganishwa na miaka minne iliyopita, kiwango cha mchezo Ice Ballet kwenye Michezo ya majira ya baridi ya China kimeinuka kwa kiasi kikubwa, na wachezaji wachipukizi wengi wamejitokeza kwenye mashindano mbalimbali. Ili kuondoa tatizo la ukosefu wa ustadi wa usanii ambalo limekuwepo kwa muda mrefu kwenye mchezo huo wa China, michezo ya kuteleza barafu kwa vitendo huria kwa mwanamume na mwanamke imeanzishwa kwenye Michezo ya majira ya baridi ya China, ili kuwahimiza wachezaji wachukue mashindano kama ni maonesho. Bw. Ren Hongguo alisema:

"Wachezaji wa China bado hawana ustadi wa kutosha wa usanii wakati wa mashindano. Lengo la kufanyika kwa michezo ya kuteleza barafu kwa vitendo huria kwenye Michezo ya majira ya baridi ya China ni kuwafanya makocha wa mchezo wa Ice Ballet waweke mkazo katika ustadi wa usanii wa mchezo huo. Na mafanikio yaliyopatikana kwenye mchezo huo yanategemea juhudi za miaka mingi."

Hivi sasa mkakati wa maendeleo ya muda mrefu wa michezo ya majira ya baridi ya China umepata maendeleo mazuri yanayowafurahisha watu. Hadi sasa miaka miwili imebaki kabla ya kufanyika kwa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya mwaka 2010. Je, wachezaji watakaoshiriki kwenye Michezo ya majira ya baridi ya China wana mipango gani wakijiandaa kwa ajili ya michezo hiyo? Bw. Ren Hongguo alisema:

"Michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi inafanyika kila baada ya miaka miwili, hivyo tunapaswa kuweka mkazo katika michezo na wachezaji muhimu ili kuinua kiwango cha timu yetu."

Idhaa ya kiswahili 2008-02-05