Rais Maduro wa Venezuela akabiliwa na maandamano ya kumtoa madarakani
Maandamano dhidi ya Rais wa Venezuela mwenye mrengo wa kijamaa Nicolas Maduro yamefanyika katika maeneo yote ya nchi hiyo, huku na baadhi waandamanaji kufanya vurugu.
Kuna taarifa kuwa vikosi vya usalama vimepambana na waandamanaji katika miji mbalimbali, huku watu kadhaa wakijeruhiwa na wengine kuwekwa kizuizini.
maandamano hayo ni ya wito wa kumtaka Rais Maduro ajiuzulu juu ya kushindwa kwake katika usimamizi wa Uchumi.
Muungano wa upinzani nchini humo umetoa masaa 12 ya maandamano ya pamoja siku ya ijumaa ili kuongeza shinikizo kwa Rais huyo kujiuzulu, ambapo wanamshutumu kwa ukiukwaji wa Demokrasia, na bunge la nchi hiyo linamshutumu kwa kutaka kupanga mapinduzi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |