UNICEF yasema watoto 145 wameachiliwa huru na makundi yenye silaha nchini Sudan Kusini
Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF limesema watoto 145 wameachiliwa huru na makundi yenye silaha kwenye eneo la utawala wa Pibor nchini Sudan Kusini, ambayo ni idadi kubwa kabisa ya watoto walioachiliwa tangu mwaka 2015.
Mjumbe wa shirika hilo nchini Sudan Kusini Bw. Mahimbo Mdoe amesema wanatarajia watoto elfu 16 wanaohudumia jeshini au makundi yenye silaha wanaweza kurudi kwenye familia yao.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |