Moto mkubwa watishia Israel
Maelfu ya watu wamelazimika kukimbia makwao baada ya moto mkubwa kuendelea kuenea na kukaribia kufika katika mji wa Haifa, kaskazini mwa nchi hiyo.
Watu karibu 50,000 katika mitaa minane wametakiwa kuhama, maafisa wanasema.
Hakujaripotiwa taarifa zozote za watu kuumia vibaya lakini watu kadha wamepelekwa hospitalini wakikabiliwa na matatizo kutokana na kupumua hewa iliyojaa moshi.
Ukosefu wa unyevu kwenye hewa pamoja na kuwepo kwa upepo mkali kumesababisha moto huo kuenea upesi.
Ndege iliyobebea maji ya kuzima moto ilipaa juu ya mji huo. Polisi wanasema wakazi wamekabiliwa na moto kutoka maeneo manne.
Katika baadhi ya maeneo ya Haifa, moto huo umeanza kukaribia sana majumba ya makazi
Maeneo yanayokabiliwa na moto huo yalikuwa yamekabiliwa na kiangazi kwa miezi miwili. Mawaziri wanasema huenda moto huo uliwashwa makusudi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |