Rais wa Zambia afanya mazungumzo na mwenzake wa Sudan Kusini kuhusu suala la usalama
Rais Edgar Lungu wa Zambia wiki hii amefanya mazungumzo na mwenzake wa Sudan Kusini Bw Salva Kiir kuhusu hali ya usalama nchini Sudan Kusini.
Viongozi hao wamefanya mazungumzo hayo kwenye mkutano wa kilele wa nchi za Afrika na za kiarabu unaofanyika mjini Malabo, nchini Guinea ya Ikweta.
Msemaji wa rais wa Zambia Bw Amos Chanda amesema rais Lungu ana matumaini makubwa na Rais Kiir kujenga nchi yenye amani. Rais Lungu ametaka vurugu nchini Sudan Kusini zikomeshwe, na kusema anaunga mkono msimamo mkali uliochukuliwa na viongozi wa Kenya na Ethiopia dhidi ya watu wanaochochea vurugu nchini Sudan Kusini.
Pia amesema Rais Lungu atawasilisha suala la Sudan Kusini kwenye mkutano ujao wa Umoja wa Afrika.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |