• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Disemba 3-9)

    (GMT+08:00) 2016-12-09 22:02:10

    Dominic Ongwen afunguliwa mashtaka 70 ICC

    Aliyekuwa kamanda wa juu katika kundi la waasi wa Uganda wa Lord's Resistance Army, LRA, Dominic Ongwen, Jumanne ya Desemba 6, amesomewa mashtaka 70 ya makosa ya kivita na uhalifu dhidi ya binadamu, mbele ya majaji wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ya ICC, iliyoko The Hague, Uholanzi.

    Awali wakati akifungua kikao cha mahakama kwaajili ya kusoma mashtaka yanayomkabili Ongwen, jaji kiongozi kwenye kesi hii, Bertram Schmitt, ametupilia mbali mapingamizi yote yaliyowasilishwa na upande wa utetezi waliotaka mteja wao kupimwa akili kwanza ili kujua ikiwa ana stahili kusimama kizimbani au la.

    Jaji Schmitt katika uamuzi wake kupitia majaji wengine wawili wanaosikiliza kesi hiyo, ameeleza kusikitishwa na upande wa utetezi kuamua kuibua masuala ambayo yangeweza kuwa yameibuliwa wakati wa mchakato wa ufunguzi wa kesi yenyewe.

    Mashtaka aliyosomewa Ongwen, yanahusu makosa ya kivita, uhalifu dhidi ya binadamu hasa kuhusu vitendo vya ubakaji, mauaji ya kiholela, kulazimisha watu kuhama makazi yao, utumikishaji wa watoto katika jeshi, udhalilishaji wa kingono na utumwa.

     

    1 2 3 4 5 6 7
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako