OPEC kuendelea kupunguza uzalishaji wa mafuta
Waziri wa nishati wa Saudi Arabia Khalid bin Abdulaziz Al Falih amesema, nchi wanachama wa Shirika la Nchi Zinazozalisha Mafuta kwa Wingi (OPEC) zitapunguza tena uzalishaji wa mafuta.
Bw. Falih amesema, kama bei ya mafuta ikiendelea kushuka kutokana na kupungua kwa mahitaji, Saudi Arabia itaweza kusaini tena makubaliano ya kupunguza uzalishaji wa mafuta kama mwaka jana.
Habari zinasema, nchi wanachama wa OPEC watakutana kwa mara nyingine mwezi Mei.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |