Rais wa Mexico asikitishwa na kulaani amri kuhusu kujengwa kwa ukuta wa mpaka kati nchi yake na Marekani
Rais Donald Trump wa Marekani jana alisaini amri mbili zinazolenga kuimarisha usalama wa mpaka na kuimairhsa sera ya uhamiaji. Usiku wa siku hiyo rais Enrique Pena Nieto wa Mexico alitoa hotuba kwenye video akisema anasikitishwa na kulaani kujengwa kwa ukuta kwenye mpaka kati ya Marekani na Mexico, na kuahidi kuwapokea wahamiaji wa Mexico nchini Marekani.
Amesema ukuta uliojengwa katika miaka mingi iliyopita haujaiunganisha Mexico na Marekani, na badala yake ulizitenganisha nchi hizo mbili. Amesema Mexico haiamini kama ukuta huo utakuwa na ufanisi, na haitalipia ukuta huo.
Rais Nieto alisema hayo kujibu amri ya rais Trump kuhusu kuimairsha sera ya uhamiaji, kuwa wizara ya mambo ya nje ya Mexico itaimarisha hatua za kulinda haki na maslahi ya wahamiaji hao.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |