DRC yaikabidhi Burundi watuhumiwa zaidi ya 128 wa uasi
Waziri wa sheria wa Burundi Aimee Laurentine Kanyana amesema, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC imewakabidhi watuhumiwa zaidi ya 128 wa uasi kwa mamlaka ya Burundi.
Makabidhiano hayo yamefanyika katika kituo cha mpaka cha Gatumba, kilomita 18 kutoka mji mkuu wa Brundi, Bujumbura, kati ya mkuu wa Mkoa wa Kivu Kaskazini nchini DRC Marcellin Cishambo na Bw. Kanyana.
Waziri huyo amesema, inaaminika kuwa vijana hao waliandikishwa na baadhi ya makundi ili kuleta tishio kwa serikali ya Burundi, na kusema huenda watu hao wanaweza kuwa waasi. Ameongeza kuwa watu hao watapewa elimu ya uraia kabla ya kurudishwa kwenye familia zao.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |