• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Januari 28-Februari 3)

    (GMT+08:00) 2017-02-03 17:48:15

    Uchaguzi wa urais nchini Somalia wavutia wagombea 24

    Tume ya uchaguzi wa rais nchini Somalia imetangaza kuwa, jumla ya watu 24 watagombea nafasi ya urais katika uchaguzi utakaofanyika tarehe 8 mwezi ujao, ikiwa ni ishara ya kufanyika kwa uchaguzi wa urais ulioahirishwa mara kadhaa.

    Tume hiyo yenye wajumbe 18 kutoka baraza la chini na la juu la bunge, imesema kuwa imewapitisha wagombea hao baada ya kufunga muda wa mwisho wa kujisajili.

    Wagombea hao ni pamoja na rais wa sasa wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud, waziri mkuu Omar Abdirashid Ali Shamarke, na rais wa zamani wa nchi hiyo Sharif Sheikh Ahmed.

    Kila mgombea atatakiwa kupata japo kura 219 ili kupata ushindi katika raundi ya kwanza, na kama ikishindikana, raundi ya pili ya upigaji kura itafanyika kati ya wagombea wanne watakaopata kura nyingi zaidi katika raundi ya kwanza.


    1 2 3 4 5 6 7 8
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako