Duru ya pili ya uchaguzi kufanyika Ufaransa
Emmanuel Macron mgombea wa mrengo wa kati na Marine Le Pen wa chama cha kihafidhina wanaongoza katika duru ya kwanza ya uchaguzi wa rais uliofanyika jana nchini Ufaransa na sasa watachuana vikali katika duru ya pili ya uchaguzi huo unaopangwa kufanyika Mei 7 mwaka huu.
Matokeo rasmi yaliyotolewa na Wizara ya mambo ya ndani ya Ufaransa wiki hii yamethibitisha kuwa mgombea Bw Emmanuel Macron mwenye mrengo wa kati ameongoza katika duru ya kwanza ya uchaguzi wa urais nchini humo.
Macron amechukua nafasi ya kwanza kuwa kupata asilimia 24.01 ya kura huku nafasi ya pili ikichukuliwa na mpinzani wake Bi Marine Le Pen, kiongozi wa chama cha mrengo wa kulia cha National Front, aliyepata asilimia 21.30 ya kura. Watagombea hawa watakutana katika duru ya pili ya uchaguzi itakayofanyika tarehe 7 mwezi ujao.
Rais Francois Hollande amesema atampigia kura Bw Emmanuel Marcon katika duru ya pili ya uchaguzi, kwa kuwa ana uwezo wa kulinda maadili yanayoruhusu umoja wa taifa katika kipindi hiki maalumu. Akihutubia taifa kupitia televisheni, rais Hollande ameonya kuwa msimamo wa kupinga uhamiaji kutoka chama cha mrengo wa kulia utasababisha mgawanyiko mkubwa wa taifa.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |