Upinzani Kenya wamteua mgombea wa urais
Vyama vya upinzani nchini Kenya ambavyo viko chini ya muungano wa National Super Alliance (NASA) vimemteua aliyekuwa waziri mkuu Raila Odinga kuwa mgombea wa urais katika uchaguzi mkuu Agosti 8 mwaka huu.
Siasa nchini humo vimepamba moto wakati ikiwa imesalia miezi 3 tu kabla ya uchaguzi huo.
Katika bustani ya Uhuru mjini Nairobi wafuasi wa muungano wa upinzani National Super Alliance (NASA) walifurika kuanzia saa kumi na mbili alhamis.
Baada ya masaa kadhaa hatimaye vigogo watano wenye vyama tanzu vya muungano huo wakafika tayari kumtangaza mmoja wao kuwa mgombea wa urais kushindana na chama tawala cha jubilee.
Kama ilivyokuwa imetabiriwa na wengi aliyekuwa waziri mkuu Raila Odinga alitangazwa mgombea na naibu wake wa rais atakuwa ni Kalonzo Musyoka.
Raila Odinga akihutubia wafuasi baada ya kukabidhiwa bendera anasema anachukua uteuzi huo kama heshima kubwa kutoka kwa wenzake.
Kulingana na makubaliano yao, Musalia Mudavadi anayeongoza chama cha Amani National Congress atakuwa waziri mkuu mratibu wa shughuli za serikali huku naye kiongozi wa Ford Kenya Moses W
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |