1-Shambulizi la Kigaidi Somalia
Watu watano wameuawa na wengine kadhaa wamejeruhiwa kwenye mlipuko wa mabomu yiliyotegwa kwenye gari mjini Mogadishu, Somalia.
Katika shambulizi moja gari lenye mabomu lilivamia kituo cha polisi cha Waberi, na shambulizi lingine lilitokea katika ofisi ya kamishna siku mbili zilizopita mjini Mogadishu na kusababisha vifo vya watu 10.
Msemaji wa wizara ya usalama ya Somalia Bw Ahmed Mohamud amesema gari hilo lenye mabomu liligonga mlango wa kituo cha polisi na kusababisha vifo na majeruhi.
Mashuhuda wamesema kituo cha redio cha Mustaqbal kilicho karibu na eneo la tukio kimesimamisha kazi baada ya shambulizi kutokea.
Hakuna kundi lolote lililotaja kuhusika na mashambulizi. Lakini kundi la Al-Shabaab limethibitisha kuhusika na mashambulizi mengine mawili yaliyotokea ndani ya wiki moja na kusababisha vifo vya watu 40.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |