7-Umaskini kupungua Duniani
Sera mpya ya shirika la Umoja wa Mataifa la elimu,sayansi na utamaduni UNESCO, inasema kwamba umasikini duniani waweza kupungua kwa nusu ikiwa watu wazima wote watahitimu elimu ya sekondari.
Wakati sera hiyo ikisema hivyo, takwimu mpya za shirika hilo zinaonyesha kuwa kumekuwa na muendelezo wa idadi kubwa ya watu kutohudhuria shule, jambo linalotoa mwelekeo kwamba ndoto hizo zaweza kutotimia kwa vizazi vingi vijavyo.
Sera hiyo mpya ifahamikayo kwa jina ,Kupunguza umasikini duniani kupitia elimu ya msingi na sekondari, imetolewa kuelekea mkutano wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa kuhusu maendeleo endelevu SDGs utakaofanyika Julai 10 hadi 19. Sera hiyo inatambua elimu kama msingi wa kukomesha umasikini.
Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Irina Bokova amesema sera hiyo ni habari njema kwa wadau wote wa maendeleo endelevu SDGs.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |